Warning: Creating default object from empty value in /data/www/africaweb/HomePage/fun/index.build.php on line 26
Ghanaweb Fun Page
Uko hapa: NyumbaniBurudaniHuman Interest

Tabloid News of Thursday 25 March 2021

Source: kiswahili.tuko.co.ke

Buda Alazimika Kufichulia Mke Kuhusu Mpango wa Kando Tapeli

Mzee mmoja tajiri mwenye afisi jijini Nairobi alilazimika kufichua siri zake za michepuko kwa mkewe ili kujinusuru kutoka kwa mpango wake wa kando aliyekuwa akimtapeli.

Hii ni baada ya mrembo huyo ambaye alikuwa amechumbiana na mzee kwa miaka saba kutishia kuanika siri zao mbele ya mkewe baada ya penzi lao kuingia doa.

Kulingana na Taifa Leo, matatizo yaliibuka baada ya kipusa kumtaka mzee kumtumia KSh 20,000 kila siku, jambo ambao lilimshtua sana buda ambaye alianza kumfokea.

“Je, umesahau ulivyojisifu tulipokutana kwa mara ya kwanza? Kwamba wewe hupokea zaidi ya elfu hamsini kila siku? Iweje ulielie kwamba nakufilisi. Tuma pesa la sivyo, najua alipo mkeo. Naweza kuenda wakati wowote naikamweleza jinsi tumekuwa tukimla kivuli miaka hiyo,” demu alitishia.

Inasemekana buda read more

More Tabloid News