Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 10 12Article 562840

Habari za Afya of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

CDC yaitaka Serikali kuimarisha huduma za afya nchini

CDC yaitaka Serikali kuimarisha huduma za afya CDC yaitaka Serikali kuimarisha huduma za afya

Tanzania na nchi nyingine barani Afrika zimetakiwa kuimarisha taasisi za afya za umma pamoja na kuongeza kasi ya zezi utoaji chanjo kama sehemu ya kutimiza malengo yaliyoekwa ya kupambana na maambukizi ya Corona.

Haya yameelezwa na Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika CDC, Dk.Joh Nkengasong wakati wa mkutano mkuu wa nane wa Afya kitaifa uliofanyika jiji Dodoma na kutoa maagizo kwa wataalam wa afya pamoja na watunga sera nchini kuja na mikakati itakayoendana na kasi ya kudhibiti ugonjwa huo.

"Tunapenda kuihamasiha Serikali ya Tanzania kuboresha zoezi hili ili kuweza kuwafikia wananchi wengi na mwisho tuweze kufikia maengo ya CDC" Amesea Mkurugenzi huyo.

Aidha amezitaka nchi zote barani Afrika kujenga mahusiano chanya baina ya taasisi za Afya za Serikali, binafsi pamoja na zile za kimataifa katika kupambana na janga hilo liloathiri dunia nzia kwa ujumla.