Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 10 13Article 563065

Habari za Afya of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

MSD kukamilisha usambazaji dawa Oktoba 16

MSD kukamilisha usambazaji dawa OKtoba 16, 2021 MSD kukamilisha usambazaji dawa OKtoba 16, 2021

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze amesema MSD inaendelea na mpango wa usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa kasi kubwa ambapo hadi kufikia Oktoba 16 hakutakuwa na kituo cha kutolea huduma za afya nchini Tanzania kitakachokuwa na uhaba wa bidhaa za afya.

Amesema agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuitaka MSD kupeleka dawa vituoni ndani ya siku saba limekuja na msukumo mkubwa na sasa MSD imeongeza masaa zaidi ya kufanya kazi hasahasa kwenye maghala ya kupokelea dawa.

Ameongeza kusema kuwa MSD husambaza dawa kwa kuzingatia mzunguko (ILS) ambao ni mara nne hadi sita kwa mwaka lakini kutokana na agizo la Waziri Mkuu, wamechukua hatua ya kupeleka dawa hizo pindi tu zinapopokelewa.

Amesema shehena nyingine za dawa tani 12 zitaingizwa Tanzania kesho Oktoba 14, 2021 alhamisi pamoja na makontena 18 ya dawa yanatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia Oktoba 15 na zitamaliza tatizo la uhaba wa dawa lililojitokeza