Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 11 26Article 574093

Habari za Afya of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

RIPOTI: Madaktari na wauguzi Afrika wanapambana na janga bila kinga ya COVID-19

Madaktari na wauguzi Afrika wanapambana na janga bila kinga ya COVID-19 Madaktari na wauguzi Afrika wanapambana na janga bila kinga ya COVID-19

Imeelezwa kuwa ni mfanyakazi mmoja tu kati ya wanne kutoka sekta ya afya barani Afrika ambaye amepewa chanjo kamili dhidi ya Covid-19, na kuacha idadi kubwa ya wafanyikazi kwenye mstari wa mbele wa janga hili bila kinga, uchambuzi wa awali wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) unaonesha.

Uchambuzi wa takwimu zilizoripotiwa kutoka nchi 25 unaonesha kuwa tangu Machi 2021, wafanyakazi wa afya milioni 1.3 barani Afrika, au asilimia 27, wamechanjwa kikamilifu.

Kinyume chake, utafiti wa hivi karbuni wa kimataifa wa WHO katika nchi 22 zenye kipato kikubwa ulionyesha kuwa asilimia 80 ya wafanyakazi wao wa afya na wahudumu wa afya wameathirika na janga hilo.

"Wahudumu wengi wa afya barani Afrika bado wanakosa chanjo na wanabaki wazi kwa maambukizo makali ya Covid-19. Isipokuwa madaktari wetu, wauguzi na wafanyikazi wengine wa mstari wa mbele wapate ulinzi kamili tunahatarisha kurudi nyuma katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima tuhakikishe vituo vyetu vya afya ni mazingira salama ya kufanyia kazi,” alisema Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.