Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 09 13Article 557167

Habari za Afya of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali imeongeza vituo 1000 vya chanjo ya COVID-19

Mkurugenzi wa huduma za kinga , Dkt. Leonard Subi Mkurugenzi wa huduma za kinga , Dkt. Leonard Subi

Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa vituo vya kutolea chanjo vimeongezeka kutoka 550 mpaka 1,548 nchini. Lengo kuu ni kuhakikisha wananchi wanapata chanjo hasa wanaoka vijini.

Ameyasema hayo akiwa jijini mwanza katika mkutano ulioendeshwa kwa njia ya mtandao ukiwa umeudhuruwa na wandishi wa habari ,wadau mbalimbali wa maswala ya Afya pamoja na vikundi vya hamasa.

Dkt Subi, amesema mpaka sasa watanzania 340,000 wameshapata chanjo na pia amewataka wanahabari waendele kutoa taarifa zilizo sahihi kuhusiana na Uviko-19 ili kusaidia kutokuwenea na habari potofu.

"Chanjo ni muhimu sana inasaidia kuimarisha kinga ya mwili , naomba tuendele kuelimisha jamii na waache kufata habari zinazotolewa na watu wasiotoka kwenye shirika la afya" , amesema Dkt Subi.

Dkt bingwa wa Magonjwa kutoka hospital ya taifa Muhimbili, Elisha Osati, ameseama watanzania wanatakiwa waache uwonga wa kuchoma chanjo na wajitokeze kwa wingi na hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa uchomaji wa chanjo umefanikiwa kupunguza idaidi ya vifo chini nyingi kama Europe, Asia na Marekani .