Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2022 01 14Article 585850

Habari za Afya of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali yapokea msaada wa dawa za minyoo

Serikali yapokea msaada wa dawa za minyoo Serikali yapokea msaada wa dawa za minyoo

Serikali imepokea msaada wa dawa kwa ajili ya kampeni ya kupambana na minyoo pamoja na kuongeza virutubisho kwenye mwili kutoka shirika la World Vision Tanzania zenye thamani ya Sh milioni 341.

Dawa hizo zimepokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Dawa na Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi kwa niaba ya Katibu Mkuu Profesa. Abel Makubi.

"Tunamshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo, mahusiano haya mazuri ndiyo yamewezesha pia kupatikana kwa msaada,” amesema Msasi.

Msasi amesema dawa hizo zinatolewa mara mbili kwa mwaka (mwezi June na Desemba) kwa lengo la kupunguza na kukabiliana na kiasi cha minyoo kwenye miili ya watoto ili wasiwe na upungufu wa damu na hivyo kusaidia kukabiliana na vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkurugenzi mwandamizi wa shirika la World Vision Tanzania Dk Joseph Mitinje amesema shirika hilo linafanya kazi na Serikali kupitia wizara zake ili kuboresha huduma mbalimbali kwa watanzania bila kujali matabaka.

"Mchango huu umepatikana kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, World Vision ya Serikali ya Marekani pamoja na World Vision ya Serikali ya Canada katika kuhakikisha dawa hizo zinapatikana".Amesema Dk Mitinje.