Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 09 13Article 557203

Habari za Afya of Monday, 13 September 2021

Chanzo: Mwananchi

TB yatajwa kuua watu 74 kila siku Tanzania

Ugonjwa wa TB Ugonjwa wa TB

Watu 74 wanakufa kila siku nchini kutokana na kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) huku idadi ya wagonjwa sugu ikiwa juu.

Idadi hiyo ni sawa na abiria wa basi lililojaa linalofanya safari wakiwa wamekaa kwenye siti na wengine kusimama kutokana na kujaza kupita uwezo.

Takwimu hizo za mwaka 2018 zilitolewa juzi na Serikali wakati wa uzinduzi wa muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunge, viongozi wa dini na taasisi nyingine za kiraia.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, wabunge vinara wa kupambana na TB, Dk Saitole Laizer alisema ugonjwa huo bado ni tishio nchini, ingawa watu wengi hawajui kuwa unaua na utaendelea kuua ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa haraka.

Dk Laizer amesema vipimo vinaonyesha kati ya watu 133,000 wanaopimwa, 227 hukutwa na maambukizi, hivyo kuifanya Tanzania kuwa ina wagonjwa 1,600 wa TB sugu, wakiwamo 400 waliogundulika mwaka jana pekee.

Hata hivyo, Dk Laizer aliyataja makundi hatarishi kuwa ni watumiaji wa dawa za kulevya na wanaojidunga sindano.

“Serikali imetupatia fedha nyingi ambazo zimefanikisha kununua magari mapya matano yaRTISEMENtakayofanya kazi hadi vijijini kwa ajili ya vipimo kwa watu wanaoshindwa kufika hospitalini, hivyo mapambano haya yanatakiwa kuwa endelevu kwa nguvu na kwa kila mmoja wetu,” alisema.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel alisema wizara imepokea Sh97 bilioni kutoka serikalini kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya TB, ikiwamo kuimarisha huduma za afya vijijini na kukusanya takwimu za wagonjwa waliopo na mwenendo wa maambukizi.

Naibu waziri huyo alisema wanatarajia kuwafikia watu wengi kwa kutumia magari hayo mapya ambayo yana kliniki zinazotembea (mobile clinic), jambo alilosema litamaliza changamoto ya ugonjwa huo na kufikisha elimu moja kwa moja kwa jamii, hasa wananchi wa vijijini kuwashirikisha kuitokomeza TB nchini ifikapo mwaka 2030.

Wakati huohuo, Dk Mollel alizungumzia muswaada wa bima ya afya kwa wote kuwa sasa umeiva, kwani hivi karibuni ulitoka mikononi mwa kamati ya makatibu wakuu na kupelekwa baraza la mawaziri ili waupitie na utawasilishwa bungeni Novemba mwaka huu.

Dk Mollel amesema Muswada huo ulikwama katika hatua moja kwa miaka minane, lakini jambo jema ni kwamba umekamilika na umepita hatua hiyo, hivyo akaomba wabunge wausubiri kuujadili na kuuboresha kabla sheria ya kuwahakikishia Watanzania matibabu haijapitishwa.

Akizungumzia uzinduzi huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema TB ni miongoni mwa magonjwa yanayoua kwa wingi Tanzania na duniani ambayo hayatakiwi kufanyiwa mchezo katika mapambano yake.

Aliwataka Watanzania kujihadhari na kuchukua hatua wanapoona kuna dalili, kwani ugonjwa unaweza kumpata mtu yeyote na wakati wowote, lakini akaomba taasisi ziwekeze fedha kwa vyombo vya habari ili elimu ya ugonjwa huo ipelekwe hadi maeneo ya vijijini wanakoishi Watanzania wengi.