Uko hapa: NyumbaniHabariHealth2021 10 27Article 566020

Habari za Afya of Wednesday, 27 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tanzania inatarajia kukamilisha utengenezaji wa Chanjo ya COVID-19

Tanzania inatarajia kukamilisha utengenezaji wa Chanjo ya COVID-19 Tanzania inatarajia kukamilisha utengenezaji wa Chanjo ya COVID-19

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza hatua ya pili ya majaribio ya chanjo ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Abel Makubi alisema jana kuwa, wanatarajia kukamilisha majaribio ndani ya miezi sita.

Alisema hayo jijini Dodoma kwenye kikao kilichokutanisha maofisa wa serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na mashirika ya dini kujadili namna ya kushirikiana kukabili Covid-19.

“Sasa hivi tumeanza kutengeneza chanjo yetu ya Covid-19 kwa kushirikiana na sekta binafsi na tupo makini kwenye hili, endapo tutafanikiwa kwenye chanjo tutakuwa tumefanikiwa kwenye sekta binafsi,” alisema.

Profesa Makubi alisema mwitikio wa watu kupata chanjo hiyo ni mkubwa na akawahimiza wananchi waendelee kuchanja chanjo ya Sinopharm.

“Tunahamasisha wananchi kujikinga na Covid- 19 hasa katika suala la chanjo, tunatambua kuwa sekta binafsi imekuwa na mchango na mkubwa imeshughulika sana katika kuwatibu, tunawaomba tuendelee kuwa pamoja kushawishi wananchi kuchanja kwa hiari kwa wingi.”

“Tunawashauri wananchi kuwa chanjo ya sasa inatolewa mara mbili, niwasisitize warudi kuchanja ndio watajenga kinga ya kutosha ukichanja mara moja ukapotea haitakukinga maana zina dozi mbili ukipata zote itakusaidia,” alisema.

Profesa Makubi alisema takwimu za hospitali zinaonesha kuwa, wanaougua ni wasiochanja hivyo kumaanisha kwamba usipochanja unaongeza uwezekano wa kumbukizwa na kuwa kwenye hali mbaya au kupoteza maisha.

Aliihimiza sekta binafsi iwekeze ili kuboresha huduma za afya nchini na akasema waliwaita washaueriane ili wawekeze katika maeneo mbalimbali vikiwamo viwanda vya dawa na kuanzisha hospitali.

Ofisa Uhamasishaji Uwekezaji Kanda ya Kati na Kaimu Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) kanda hiyo, Juma Zima alisema kuna fursa kuwekeza kwenye uzalishaji dawa, vifaa tiba, vituo vya afya na hospitali.

"Faida ya kuwekeza hapa nchini ni kubwa sana kwa sababu mahitaji ni makubwa, soko kubwa na kubwa zaidi manufaa ya kikodi katika maeneo mengi ikiwamo uingizaji wa mitambo au bidhaa za mtaji kwa wawekezaji wa viwanda vya sekta ya afya ni bure na vifaa vya tiba vimeondolewa kabisa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)," alisema Zima.

Ofisa Mwandamizi Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), Panduka Yonazi alisema serikali imejenga miundombinu na kurahisisha huduma za kumsaidia mwenye viwanda kuwekeza