Uko hapa: NyumbaniHabariHealthAfya

 

 

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

_____

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

SERA YA AFYA

Juni, 2007

TAFSIRI

Neno

Tafsiri

Afya

Ukamilifu wa binadamu kimwili, kiakili na kijamii na kutokuwepo kwa maradhi

Bioanuai

Aina mbalimbali za maisha ya viumbe hai, jinsi vinavyoishi katika mifumo ya maisha.

Chembe hai na viini tete

Chembe hai ni seli na Viini tete ni viini vilivyobadilishwa kijenetiki, vinavyoweza kuhifadhiwa na kurutubishwa kwa ajili ya kupata kiumbe kipya pasipo kukutana kwa mbegu ya kiume na yai la kike. Vile vile, viini tete hivyo vyaweza kutumika kutibu magonjwa kama kansa na ukuaji usio kawaida wa chembe hai (abnormal growth).

Huduma za utengemao

Humaanisha huduma zinazomwezesha mtu mwenye matatizo ya kijamii, kumudu maisha yake ya kila siku na pia kushiriki kikamilifu katika kuiletea maendeleo jamii inayomzunguka.

Ithibati

Ni hati ya kutambulika baada ya kufikia viwango vilivyowekwa.

Masuala mtambuka

Ni yale ambayo utekelezaji wake unagusa sekta mbalimbali na jamii.

Matamko

Ni azma ya Serikali inayoelekeza kufikia malengo iliyojiwekea.

Sera

Ni tamko lenye kusudio la kufikia lengo au madhumuni maalum.

Taaluma mseto

Kuwa na wataalam wenye taaluma mbalimbali katika kituo cha kutolea huduma za afya.

TEKNOHAMA

Ni kifupisho cha ‘Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.’

Tofauti kati ya upungufu na changamoto

Upungufu ni tatizo lililopo na changamoto ni namna ya kukabiliana na tatizo.

 

DIBAJI

Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao. Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali.

Katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

Sera ambayo imeendelea kutumika katika kuelekeza utoaji wa huduma za afya ilipitishwa mwaka 1990. Tangu sera hiyo ilipopitishwa, yamekuwepo mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, mabadiliko ya sayansi na technolojia na kuongezeka kwa magonjwa. Yametokea pia, maelekezo mbalimbali ya Serikali. Mabadiliko na maelekezo yote haya yanatoa changamoto mpya katika utoaji wa huduma za afya na yamechangia kwa pamoja kuifanya sera iliyopitishwa mwaka 1990 kutokidhi mahitaji na matarajio ya sasa na ya miaka ijayo.

Mfumo na utaratibu wa utoaji huduma unaotumika hivi sasa umebadilika kutokana na mabadiliko yaliyotokea, ikilinganishwa na mfumo uliokuwa unatumika kwa maelekezo ya Sera ya 1990. Mwaka 1996 marekebisho ya sera yalipitishwa kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa utoaji na uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi ya wilaya. Katika marekebisho haya, ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa afya ulitambuliwa na kupewa msukumo, pia yalikasimu usimamizi wa utekelezaji katika mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kuongeza ushiriki wa wananchi katika kusimamia na kumiliki raslimali za afya.

Mabadiliko haya yamelazimu kufanyia mapitio ya Sera ya mwaka 1990, na yamezingatia sera na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA).

ix

Sera ya afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka 2007, imeweka bayana dira, makusudio, maelekezo ya Serikali katika mfumo wa matamko, mabadiliko ya kiuchumi na kijamii, matokeo ya tafiti na majaribio na uzoefu katika utoaji wa huduma. Aidha, utayarishaji wa sera hii umekuwa shirikishi kwa Wizara kuwashirikisha wadau mbalimbali wanaotoa na kutumia huduma za afya katika kupitia Sera ya 1990.

Jukumu la wadau wote wa sekta ya afya ni kusoma, kuielewa na kutafsiri matamko yaliyomo katika sera hii wakati wa kupanga, kutoa na kutathmini huduma za afya nchini.

Wizara inatoa shukrani kwa wadau wote walioshiriki kutoa maoni yao na hivyo kukamilisha Sera hii. Nina imani kuwa wadau katika ngazi zote watashiriki kikamilifu katika kutekeleza Sera hii kwa lengo la kuboresha huduma za afya kote nchini.

Prof. David Homeli Mwakyusa (Mb),

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

x

SERA YA AFYA

UTANGULIZI1.0

Afya maana yake ni hali ya ukamilifu kimwili, kiakili, kijamii na kutokuwepo kwa maradhi. Afya bora ni nguzo na raslimali muhimu katika kuchangia maendeleo ya mtu binafsi, familia na nchi hususan katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini. Kwa mantiki hii afya inalenga kuwa na ustawi endelevu kwa jamii, kwa kuzingatia mchango wa mtu binafsi kulingana na nafasi, uwezo na fursa zilizopo katika kuleta maisha bora. Upatikanaji wa afya bora unahitaji uwezeshaji wa jamii iwe na uwezo wa kushiriki, kuamua, kupanga na kutekeleza mikakati yao ya kuwaletea maendeleo katika ngazi mbalimbali.

Mara baada ya Uhuru (1961) hadi mwaka 1990, Wizara ya Afya imetekeleza huduma za afya nchini kwa kutumia sera ya nchi kwa ujumla bila kuwepo sera rasmi ya Taifa ya Afya. Sera ya nchi ilikuwa ni kupambana na maradhi, ujinga na umaskini. Kwa hiyo mipango yote ya sekta ya afya ililenga katika kupunguza maradhi na vifo kwa kutumia raslimali zilizopatikana.

Sera rasmi ya Afya ilitayarishwa na kupitishwa mwaka 1990. Msisitizo wa sera hii ulikuwa ni kuinua hali ya afya kwa wananchi wote na kipaumbele kilitolewa kwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuugua, ambayo ni; watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito na wananchi wote. Aidha, sera ililenga kuweka mfumo wa huduma za afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa watanzania.

Sera ya Afya ya mwaka 1990 ina upungufu kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea, maelekezo mapya ya Serikali, kuongezeka kwa magonjwa yakijumuisha mapya na sugu yanayohitaji tiba ya muda mrefu, magonjwa yanayojitokeza uzeeni na mabadiliko katika sayansi na teknolojia. Hivyo, imelazimu kufanya mapitio, ili kuwa na sera inayokidhi mahitaji ya sasa na baadaye.

Sera hii ya Afya ya mwaka 2007, imetayarishwa kwa kuzingatia mabadiliko ya Sera za kiuchumi na kijamii yaliyojitokeza kitaifa na kimataifa. Misingi ya sera hii ni pamoja na Sera ya Afya ya mwaka 1990, Mabadiliko katika Sekta ya Afya, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania.

1

2.0 HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Huduma za afya nchini zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na mabadiliko endelevu yanayofanyika katika Sekta ya afya kwa lengo la kuleta uwiano katika upatikanaji wa huduma bora za afya mijini na vijijini. Kiasi cha asilimia themanini ya watanzania kufikia miaka ya tisini, tayari wana fursa ya kupatiwa huduma katika umbali wa kilomita kumi. Hata hivyo, hali ya afya ya wananchi wengi imeendelea kuwa ya wastani kutokana na changamoto zinazoendelea kujitokeza kabla na baada ya uhuru katika mfumo wa huduma za afya. Hali hii imesababisha kupungua kwa kasi ya kufikia malengo yaliyotarajiwa na serikali.

2.1 Huduma za Afya Kabla na Baada ya Uhuru

Kabla ya Uhuru, huduma za afya nchini zilikuwa zinatolewa zaidi kwenye maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashamba makubwa. Baada ya uhuru, Serikali iliweka msukumo zaidi katika kupanua huduma za afya ili kuwafikia wananchi wengi hasa walioko vijijini. Ili kufanikisha azma hii, Serikali iliweka mfumo wa rufaa wa huduma za afya. Kwa mfumo huu, zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za mikoa, maalum, kanda na taifa zilianzishwa.

Aidha, Serikali ilihamasisha na kuwezesha hospitali za mashirika ya kidini kushirikiana nayo kutoa huduma kwa wananchi. Kipaumbele kilikuwa katika utoaji wa huduma za tiba zaidi kuliko kinga.

Katika kipindi chote hicho hadi miaka ya tisini, huduma za afya zilitolewa bila malipo. Kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, Serikali ilianzisha mabadiliko katika Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika kuchangia gharama za huduma za afya mwaka 1993. Hata hivyo, makundi maalum ambayo ni; wazee wasiojiweza, watu wenye ulemavu, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito hawachangii. Serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya kwa kushirikisha sekta binafsi.

Hali ya afya ya wananchi wa Tanzania imeendelea kuboreshwa baada ya Uhuru. Hata hivyo kuna baadhi ya makundi ya wananchi ambayo yanahitaji kupewa kipaumbele ili kuendelea kuboresha afya zao kwa kuimarisha mfumo wa utoaji huduma. Wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 51, yaani miaka 50 kwa wanaume na 52 kwa wanawake. Juhudi zilizopo zitaendelea kuboresha wastani huo.

2

Watanzania wanakabiliwa na magonjwa makubwa ya kuambukiza ambayo ni UKIMWI, malaria na kifua kikuu. Aidha, afya ya uzazi na mtoto bado hairidhishi. Vile vile, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameanza kujitokeza kwa wingi kutokana na mabadiliko ya mienendo na tabia ya kuishi. Magonjwa haya ni kama saratani, shinikizo la damu, kiharusi na kisukari.

2.2 Utekelezaji wa Sera ya mwaka 1990

Sera ya mwaka tisini ilitoa kipaumbele katika utoaji huduma za kinga, tiba, uhamasishaji na utengemao. Huduma hizi zilitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Katika kutoa huduma za kinga, Serikali imeelekeza mapambano yake katika kutokomeza magonjwa yanayosababisha vifo vya watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja na miaka mitano na wanawake wajawazito. Katika utoaji wa huduma hizo, msisitizo umeelekezwa katika utoaji wa chanjo, elimu ya afya na kuruhusu upatikanaji huduma hizo bila malipo. Aidha, Serikali inaendelea na jitihada za kudhibiti na kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Huduma za tiba zimeendelea kutolewa katika ngazi zote. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa; dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vinapatikana na kusambazwa katika vituo vyote vya kutolea huduma. Serikali pia, kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika ngazi zote. Katika kuboresha huduma, mafunzo mbalimbali yamekuwa yakitolewa kwa watumishi kufuatana na taaluma zao na mahitaji. Vilevile, Serikali imeendelea kutoa huduma kwa makundi maalum. Aidha, jamii imeendelea kushirikishwa kikamilifu katika kutambua, kupanga na kutekeleza mipango ya afya ikiwemo usafi wa mazingira na usafi wa mtu binafsi.

Serikali imeendelea kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, kwa kuanzisha na kutekeleza mikakati maalum ya kuelimisha jamii ili kupunguza maambukizi mapya, kujikinga na kuchukua hatua ya matibabu sahihi mapema. Serikali pia, imekuwa inaendeleza huduma za utengemao kwa kutoa vifaa vya kujimudu, elimu ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kujitegemea na kutoa huduma za tiba na kinga.

2.2.1 Mafanikio

Utekelezaji wa mipango na mikakati ya huduma za afya na ustawi wa jamii umeleta mafanikio katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama ifuatavyo: -

Wananchi wameelimishwa juu ya umuhimu wa huduma za afya na (i) kuhamasishwa kutumia huduma hizo, hali ambayo imechochea mahitaji

3

makubwa kwa kila ngazi na kila sehemu ya nchi;

Ushirikishwaji wa wananchi katika huduma za afya umewezesha (ii) kuongezeka kwa vituo vya Serikali na binafsi na kuchochea mahitaji makubwa ya watumishi na kupanua vyuo ili kuongeza idadi ya wanaojiunga;

Uwezo, uzoefu na mifumo ya kutoa huduma ya mama na mtoto na ya (iii) kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza yakiwemo maradhi makuu kama vile malaria, kifua kikuu na UKIMWI umejengwa na kuimarika;

Sheria mbalimbali zimetungwa na nyingine kufanyiwa mapitio kutokana (iv) na mabadiliko katika Sekta ya Afya kwa lengo la kuboresha usimamizi wa huduma za Afya nchini na kulinda afya za wananchi.

2.2.2 Upungufu

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, katika utekelezaji wa sera ya 1990 bado kuna upungufu katika kufikia malengo yaliyokusudiwa kama ifuatavyo: -

Sera hiyo haikuweza kuweka mifumo ya kutosheleza mahitaji ya (i) huduma za afya kwa ngazi mbalimbali katika maeneo mengi ya nchi yetu, kwa mfano usambazaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba;

Uhaba wa wataalam wa kada mbalimbali, vifaa, dawa, vitendanishi na (ii) vifaa tiba katika sekta ya Afya;

Kukosekana kwa vivutio maalum kwa wataalam, vya kuwahamasisha (iii) kubaki katika vituo vya huduma na maeneo mbalimbali ya nchi;

Changamoto ya maendeleo na mabadiliko ya tabia na mwenendo wa (iv) maisha imebadili sura ya magonjwa. Aidha, hali hii imesababisha kuanza kujitokeza kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na yanayotokana na ajali na majanga, ambayo kwa huduma zilizopo haziwezi kukidhi;

Wananchi wengi wanaendelea kusumbuliwa na magonjwa ambayo (v) hayakupewa umuhimu, kwa mfano matende, ngirimaji, kichocho na vikope. Wakati huo huo, magonjwa mapya yameanza kujitokeza kwa nguvu, kwa mfumo wa milipuko, mfano; homa ya bonde la ufa, homa ya mafua ya ndege ambapo mfumo wa huduma uliopo haukidhi mahitaji;

4

Baadhi ya magonjwa yaliyojitokeza kwa mfano; UKIMWI, yameibua (vi) mahitaji maalum katika dhana ya lishe bora na huduma za utengemao.

2.2.3 Changamoto

Changamoto ambazo sekta ya afya inakabiliana nazo katika kutoa huduma ni kama ifuatavyo:

Namna ya kuongeza watumishi, ili kukidhi mahitaji ya sekta ya afya (i) katika ngazi zote;

Jinsi ya kuongeza bajeti ya sekta ya afya katika ngazi zote hadi kufikia (ii) kiwango kisichopungua asilimia 15 ya bajeti yote ya Serikali, kama ilivyopitishwa na Azimio la Abuja;

Kasi ya maambukizi mapya na athari za UKIMWI katika jamii (iii) ikizingatiwa kuwa asilimia 7 ya Watanzania wameambukizwa virusi vya UKIMWI;

Kuhakikisha kuwa vifo vya watoto wachanga, wenye umri chini ya (iv) mwaka mmoja, vinapungua zaidi ya 68 kwa watoto 1000 waliozaliwa hai;

Kupunguza viwango vya utapiamlo kwa watoto wenye umri chini ya (v) miaka mitano;

Kupunguza viwango vya vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi;(vi)

Kupunguza ongezeko kubwa la watoto yatima na walio katika mazingira (vii) magumu;

Kupandisha ari ya utendaji kazi wa watumishi wa sekta ya afya kutokana (viii) na mishahara midogo, ukosefu wa motisha na upungufu wa vitendea kazi;

Kudhibiti athari za utandawazi na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya (ix) sayansi ya afya;

Kudhibiti ongezeko kubwa la bei za dawa, vifaa na vifaa tiba;(x)

Kudhibiti ongezeko la vimelea vya magonjwa kuwa sugu kwa dawa (xi) zinazotumika;

Kudhibiti ongezeko la magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yakiwemo; (xii) kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na ajali;

5

Kuzuia kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza yaliyoonekana (xiii) kudhibitiwa huko nyuma;

Kuongeza ushiriki wa wananchi katika usafi wa mazingira, kama njia ya (xiv) udhibiti wa magonjwa ya kuambukizwa;

Kupambana na kuzuka kwa magonjwa mapya duniani kama vile; (xv) ugonjwa wa Kichaa cha ng’ombe unaoathiri binadamu, homa ya Mafua ya ndege, Ebola na SARS;

Kukidhi matarajio ya wananchi kwa kuwa na huduma bora za afya;(xvi)

Udhibiti wa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wa afya na (xvii) ubinafsi katika utoaji wa huduma;

Utendaji na uwajibikaji unaogongana katika ngazi mbalimbali za kutolea (xviii) huduma na maamuzi;

Mfumo thabiti wa kuhudumia wastaafu, wategemezi wao na wazee;(xix)

Kupunguza utegemezi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kutoka (xx) nje ya nchi;

Mfumo madhubuti na endelevu wa kuendeleza watumishi katika sekta (xxi) ya afya;

Usimamizi bora na endelevu wa Sekta binafsi zinazoongezeka kwa kasi (xxii) nchini;

Kuongezeka kwa ugonjwa wa malaria na usugu wa vimelea vya ugonjwa (xxiii) huo ambao unachangia zaidi ya asilimia 40 ya wagonjwa wote wa nje na asilimia 38 kwa wagonjwa wote wanaolazwa;

6

3.0 UMUHIMU WA SERA

Sera ya mwaka 1990, ambayo imekuwa ikitumiwa hadi sasa haikidhi mahitaji ya sekta ya afya kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza na yanayoendelea kujitokeza ya kiuchumi na kijamii, kuongezeka kwa magonjwa mapya na yanayojirudia kama; UKIMWI na Kifua Kikuu, uanzishaji wa utaratibu wa mfumo wa wananchi kuchangia huduma za afya na kuanzishwa kwa utaratibu wa wananchi kuwa na madaraka ya kushiriki katika kutoa maamuzi na kumiliki raslimali za sekta ya afya. Sababu nyingine zilizochangia Sera ya mwaka 1990 kutokidhi mahitaji ya sasa na wakati ujao, ni pamoja na kuwepo kwa maendeleo mapya ya sayansi na teknolojia, utekelezaji wa dira na mikakati ya taifa na utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ikiwemo Malengo ya Milenia.

Sera hii iliyopitiwa, inazingatia masuala yote yaliyotajwa hapo juu na pia, ni mwendelezo wa utekelezaji wa malengo yalioanishwa katika Sera ya mwaka 1990. Aidha, Sera hii ni muhimu kwani inatoa maelekezo ya jinsi ya kuanzisha, kuendesha na kutoa huduma za afya nchini kwa lengo la kuhakikisha kwamba kila mtu anapata huduma za afya zilizo bora na zenye uwiano na haki. Serikali inatambua kwamba wananchi walio na afya bora ni raslimali kubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Aidha, sera inalenga katika kuwezesha ushirikishwaji wa wananchi na wadau katika utoaji wa huduma za afya.

7

4.0 DIRA, MAKUSUDIO NA MADHUMUNI YA SERA

4.1 Dira

Kuwa na jamii yenye afya bora na ustawi ambayo itachangia kikamilifu katika maendeleo binafsi na ya nchi.

4.2 Makusudio

Kutoa huduma muhimu za afya zenye uwiano wa kijiografia, viwango vya ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu.

4.3 Madhumuni

Kuinua hali ya afya ya wananchi wote na hasa wale walioko kwenye hatari zaidi, kwa kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa watanzania.

4.3.1 Madhumuni mahsusi

Kupunguza magonjwa na vifo, ili kuongeza umri wa kuishi wa (i) watanzania wote kwa kutoa huduma bora za afya, pamoja na kuzingatia mahitaji ya makundi maalum, hususan; watoto wachanga na walio chini ya umri wa miaka mitano, watoto walio katika umri wa kuanza shule na walio shuleni, vijana, watu wenye ulemavu, wanawake walio katika umri wa uzazi na wazee.

Kuhakikisha kuwa huduma za afya ya msingi zinapatikana na kutolewa (ii) na mfumo madhubuti na kushirikisha jamii, kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

Kukinga na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya (iii) kuambukiza, hususan; Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu, magonjwa yatokanayo na lishe duni, afya ya mazingira, na sehemu za kazini na usimamizi wa kemikali.

Kuhamasisha wananchi kuhusu maradhi yanayoweza kuzuilika, ili (iv) waweze kuyatambua na kutafuta mbinu za kuyadhibiti.

Kumuelimisha kila mwananchi, aelewe kuwa anawajibika moja kwa (v) moja kutunza afya yake na ile ya familia yake.

8

Kujenga ushirikiano kati ya sekta ya umma, sekta binafsi, mashirika ya (vi) dini, asasi za kijamii na jamii katika kutoa huduma za afya.

Kupanga, kutoa mafunzo na kuongeza idadi ya wataalam wa afya , (vii) wenye taaluma inayokidhi viwango kwa kuzingatia usawa wa kijinsia ili kutoa huduma za afya kwa jamii katika ngazi zote.

Kuainisha, kukarabati miundombinu kwa kuzingatia mahitaji ya watu (viii) wenye ulemavu, na kuweka mfumo wa kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya, vifaa na vitendea kazi.

Kufanya mapitio na kutathmini Sera ya Afya, Miongozo, Sheria na (ix) viwango vya utoaji huduma za afya.

9

5.0 HOJA ZA SERA NA MATAMKO

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wengine, ina jukumu la kuinua hali ya afya na ustawi kwa wananchi wote, kwa kuzuia au kupunguza maradhi, ulemavu na vifo na kuwa na afya thabiti kimwili, kiakili na kijamii.

Ili kufikia azma hiyo, Wizara inalo jukumu la kuandaa sera, miongozo na mapendekezo ya sheria zitakazosaidia utoaji na usimamizi wa huduma za uboreshaji afya (Promotive), kinga, tiba na utengamao. Pia, maendeleo ya wataalam wa afya, upatikanaji na usimamizi wa raslimali watu, fedha, vifaa, miundombinu, mipango bora ya afya, yenye viwango vinavyo kubalika na zinazowafikia wananchi wote. Aidha, Wizara ina jukumu la kuboresha mahusiano na ushirikiano na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo katika utoaji wa huduma za afya.

Sera hii inatoa maelezo, madhumuni na matamko ya suala kuhusu utoaji wa huduma za afya nchini katika kila eneo muhimu la huduma za afya kama ifuatavyo: -

5.1 Afya ya Msingi

(a) Maelezo

Mkakati wa Afya ya msingi ulilenga kuimarisha afya za wananchi kuanzia ngazi ya kaya, hadi taifa kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe. Mkakati huu ulilenga kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa wananchi wote na ulitoa kipaumbele katika uboreshaji afya, kinga na tiba. Maeneo yaliyozingatiwa katika uboreshaji wa afya ni elimu ya afya, uhamasishaji wa lishe bora, afya ya mazingira na afya mashuleni; kinga ni huduma za mama na mtoto, chanjo dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na tiba ni matibabu kwa maadili ya kawaida na majeraja, dawa muhimu, huduma ya afya ya akili, kinywa na macho.

Tanzania ilikuwa nchi mojawapo duniani ambayo ilitekeleza huduma za afya ya msingi kwa mafanikio makubwa sana baada ya uhuru. Uhamasishaji na ushirikishwaji wa wananchi katika kutambua na kujitatulia matatizo yao ya afya uliimarika na kuwa mfano kwa nchi nyingine katika bara la Afrika.

Hata hivyo, kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, uwezo wa Serikali na ule wa wananchi wa kuchangia katika huduma hii muhimu umepungua sana na

10

kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama; kipindupindu, kuhara, homa ya matumbo ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kuzagaa kwa uchafu katika jamii, umeibua hoja ya kuipanua dhana ya afya ya msingi, ili iweze kukidhi mahitaji ya wakati uliopo na ujao.

(b) Madhumuni

Kupanua dhana ya afya ya msingi na kuwa na huduma bora za afya zinazoendana na wakati, endelevu na zinazowafikia wananchi wote.

Tamko la sera(c)

Serikali itashirikisha wananchi na sekta mbalimbali katika kuimarisha (i) huduma za afya katika ngazi zote ili kuboresha afya.

Serikali itaimarisha uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya.(ii)

Serikali itaimarisha mfumo uliopo wa kuongeza umiliki na sauti ya (iii) wananchi katika utoaji wa huduma za afya.

Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kwa (iv) ujumla itaweka mazingira mazuri ya kuwezesha jamii kubuni njia na mikakati mbalimbali ya kuboresha afya yao.

Serikali itatoa maelekezo kwa kamati za Mamlaka za Serikali za Mtaa (v) ili itekeleze na kusimamia huduma za afya ya msingi katika maeneo yao.

5.2 Uboreshaji na Udumishaji wa Afya

Huduma za afya kwa njia ya elimu, uhamasishaji na uragibishi zitaimarishwa na kuboreshwa katika ngazi zote na kipaumbele kitatolewa katika masuala ya lishe na mazingira.

5.2.1 Elimu ya afya

(a) Maelezo

Elimu ya afya na uhamasishaji ni njia mojawapo muhimu katika utoaji wa huduma za afya. Njia hii inatumia utaalamu wa mawasiliano na kutayarisha na kuwasilisha ujumbe mbalimbali kwa mtu binafsi, familia na jamii kwa lengo

11

la kubadilisha mienendo na tabia zinazochangia kuwepo au kutokuwepo kwa maradhi katika jamii. Mbinu mbalimbali kama vyombo vya habari, mabango, vipeperushi, majarida, vitabu na wavuti hutumika kushawishi na kuwasilisha ujumbe huo. Katika utekelezaji wa elimu ya afya na uhamasishaji, serikali imefanikiwa kutoa elimu ya afya kwa wananchi pamoja na kuwahamasisha namna ya kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Magonjwa mengi yamedhibitiwa, hasa yale yanayoweza kuzuilika kwa chanjo.

Hata hivyo, elimu ya afya inayotolewa bado haijaleta mabadiliko makubwa ya tabia na mienendo inayotarajiwa katika jamii. Aidha, mazingira yaliyopo kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa hayatoshelezi kila mtu kuweza kukuza, kulinda na kuendeleza afya yake.

(b) Madhumuni

Kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha kila mtu kulinda na kuendeleza afya yake kwa ufanisi.

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaimarisha utoaji wa (i) elimu ya afya, ili kumhamasisha na kumwezesha kila mtu kujenga tabia inayozingatia kanuni za afya na maisha bora.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa sheria, miongozo na (ii) mikakati ambayo itakayowezesha kila mtu kupata elimu, ili kulinda, kukuza na kuendeleza afya bora.

5.2.2 Uhamasishaji na Ushirikishaji

(a) Maelezo

Uhamasishaji na ushirikishaji ni mbinu inayotumika katika kushawishi mtu mmoja mmoja, makundi na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kushiriki katika kulinda, kuendeleza na kudumisha afya bora. Tangu uhuru, Serikali imeendelea kutumia uhamasishaji kama mbinu muhimu ya kuwafanya watu kubadili tabia, ili waweze kufuata kanuni bora za afya na kulinda afya zao. Uhamasishaji huu unajikita zaidi katika masuala muhimu ya afya, ambayo ni pamoja na; elimu ya afya kwa umma, lishe bora, ushirikishwaji jamii na usafi wa mazigira.

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na; udhibiti wa magonjwa, watu wengi wamehamasika kuhusu afya zao na kuchangia kikamilifu katika

12

kupambana na magonjwa ya milipuko kwa kuweka mazingira safi, kutumia maji yaliyochemshwa, kutunza afya binafsi, kuepuka tabia mbaya ya kuvuta sigara, kutumia chumvi iliyowekwa madini na uchimbaji, pamoja na kutumia vyoo.

Hata hivyo, pamoja na mafaniko hayo uhamasishaji wa wananchi katika kudumisha afya bora na endelevu katika jamii ni wa kiwango cha chini. Magonjwa ya milipuko pamoja na uchafuzi wa mazingira yameendelea kuwepo.

Aidha, viwango vya utapiamlo katika jamii viko juu pamoja na ushiriki wa wananchi katika masuala ya afya kuwa ni kiwango cha chini. Kwa hiyo, juhudi zaidi za uhamasishaji zinapaswa kuchukuliwa, ili wananchi waweze kulinda na kudumisha afya bora na endelevu.

(b) Madhumuni

Kuhamasisha jamii, ili iweze kuweka mazingira yatakakayowezesha kila mtu kulinda, kuendeleza na kudumisha afya bora, ikiwa ni pamoja na; lishe bora na kuweka mazingira katika hali bora na endelevu.

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikisha wadau mbalimbali itaimarisha utoaji wa (i) elimu ya afya, ili kumhamasisha na kumwezesha kila mtu kujenga tabia inayozingatia kanuni za afya na maisha bora.

(ii) Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaandaa na kusimamia sheria, miongozo, kanuni na mikakati ya afya, lishe na usafi wa mazingira ambayo itamwezesha kila mtu kulinda, kutunza na kuendeleza afya yake.

(iii) Serikali itaweka na kusimamia viwango vya lishe.

(iv) Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itahamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala yote yanayohusu afya, ikiwa ni pamoja na; kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini huduma za afya katika jamii zao.

5.2.3 Afya ya Mazingira

(a) Maelezo

Afya ya mazingira ni majumuisho ya juhudi mbalimbali zinazotumika katika kuweka makazi na sehemu za kazi pamoja na mandhari katika hali ya usafi. Asilimia kubwa ya magonjwa mengi yanayoathiri afya ya jamii yanatokana na uduni na uchafuzi wa mazingira na tabia duni za kiafya. Katika kukabiliana

13

na hali hii, elimu na kampeni mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa wananchi wote kwa kutumia mbinu mbalimbali. Halmashauri nyingi za miji zinasimamia utekelezaji wa usafi wa mazingira. Aidha, kumekuwepo na kupungua kwa maradhi ya milipuko katika baadhi ya maeneo nchini.

Pamoja na juhudi hizi, bado kuna upungufu katika mfumo wa kulinda na kuimarisha afya ya mazingira pamoja na kuwa na maeneo ya mazishi. Maeneo ambayo yamekuwa na upungufu mkubwa ni pamoja na; kutokuwepo kwa vyoo bora vinavyokidhi mahitaji ya kiafya, udhibiti duni wa taka ngumu na taka maji zitokanazo na huduma ya afya, ushiriki duni wa jamii na sekta binafsi, pamoja na uchafuzi wa mazingira unaosababisha kuzaliana kwa wadudu na wanyama wanaoleta maradhi.

(b) Madhumuni

Kulinda afya ya jamii kwa kuboresha usafi wa mazingira ulio endelevu.

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha jamii inazingatia (i) kanuni za usafi wa mazingira.

Serikali itaimarisha mfumo wa utupaji na uteketezaji salama wa taka (ii) zitokanazo na huduma ya afya, ikiwa ni pamoja na; dawa, vifaa, vifaa tiba, kemikali na vitendanishi vya maabara vilivyoharibika au kuisha muda wake.

Kwa kushirikiana na Halmashauri za miji na wadau wengine Serikali (iii) itasimamia utaratibu na ubora wa maeneo yanayokidhi mahitaji ya mazishi

5.2.4 Afya kazini

Wizara inatambua uwepo wa Wakala wa Serikali wa kusimamia usalama na afya ya wafanyakazi ambao wamepewa jukumu la kusimamia afya na usalama wa wafanyakazi kazini. Aidha, wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na wakala hao.

5.2.5 Lishe

Maelezo (a)

Lishe ni majumuisho ya hatua mbalimbali tokea chakula kinapoliwa na jinsi

14

miili yetu inavyochukua virutubisho na kuvitumia katika kumpatia mlaji afya bora. Lishe bora kutokana na ulaji unaofaa, yaani; chakula cha kutosha, na cha mchanganyiko chenye virutubishi katika uwiano unaotakiwa. Lishe duni hasababisha utapiamlo ambao huleta madhara ya kiafya.

Serikali imetakiwa kuweka msisitizo katika kuboresha lishe na afya za wananchi wake. Hata hivyo, juhudi za Serikali za kuhamasisha na kuelimisha jamii umuhimu wa lishe bora bado hazijapata mafanikio ya kuridhisha. Viwango vya utapiamlo bado viko juu. Hali hii, inahitaji juhudi zaidi, ili tupunguze utapiamlo katika jamii.

Madhumuni (b)

Kuimarisha na kuboresha huduma za lishe nchini.

Tamko la sera(c)

(i) Serikali itaweka mazingira mazuri kwa wadau kushiriki katika kuboresha huduma za lishe

5.3 Kinga

5.3.1 Udhibiti wa magonjwa

Maelezo (a)

Kinga ni njia kuu ya huduma za afya inayotumika katika kuzuia magonjwa yasitokee katika jamii. Tangu Uhuru nchi ya Tanzania imetilia mkazo zaidi kinga na kuzingatia usemi unaosema Kinga ni bora na rahisi kuliko tiba. Kwa kutumia njia hii magonjwa mengi ya kuambukiza katika jamii kwa mfano; Kipindupindu, kuhara damu, surua, homa ya uti wa mgongo na ugonjwa wa kupooza yaliweza kupungua kwa kiasi kikubwa.

Aidha, baadhi ya magonjwa yalitokomezwa kabisa kwa mfano ndui. Hata hivyo, bado kuna magonjwa yaliyopo na magonjwa mapya yanayoibuka na yanayojirudia ambayo husababisha vifo na ulemavu. Kwa hiyo jitihada zaidi zinahitajika ili kuweza kudhibiti hali hii na kuwezesha jamii kuwa na afya njema.

(b) Madhumuni

Kuimarisha ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma za kinga ili kuzuia maradhi na ulemavu na hivyo kupunguza vifo na gharama za kutibu magonjwa.

15

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na jamii na wadau wengine itaimarisha (i) huduma za kinga zilizo na ubora, zinazojitosheleza na kutolewa kwa usawa na uwiano.

Serikali itaimarisha na kudumisha mazingira mazuri, ili wananchi (ii) waweze kulinda na kutunza afya zao, kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya stadi za maisha na afya ya mazingira.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na mashirika ya (iii) kimataifa itaimarisha udhibiti na uzuiaji wa magonjwa, hasa yale yanayoweza kuingizwa kutoka nje ya nchi kupitia bandarini na mipakani.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka utaratibu wa kuchunguza (iv) na kutibu magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ajali katika ngazi zote.

5.3.2 Magonjwa ya kuambukiza na milipuko

(a) Maelezo

Magonjwa ya kuambukiza kama vile UKIMWI, Kifua kikuu, malaria, mengineyo pamoja na milipuko kama vile kipindupindu, tauni na surua yanaendelea kuwa ni tatizo la kiafya kwa jamii katika nchi. Aidha, magonjwa mapya na yale yanayojirudia kama vile, Ebola, Mafua ya ndege, Homa ya Bonde la Ufa na Kifua Kikuu yameongezea tatizo.

Jitihada kubwa imetumika katika kudhibiti na kupambana na magonjwa haya, kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile; kutoa elimu ya afya na uhamasishaji kwa umma, kuimarisha huduma za chanjo pamoja na kampeni, kuelimisha watumishi, kuimarisha utambuzi na tiba pamoja na ufuatiliaji wa wagonjwa. Hata hivyo, pamoja na jitahada hizi, bado magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya milipuko, mapya na yanayojirudia yanaendelea kuwa tatizo kubwa la kiafya kwa jamii.

(b) Madhumuni

Kuimarisha, kubuni na kuboresha mbinu mbalimbali za kudhibiti na kuzuia magonjwa ya kuambukiza, milipuko na magonjwa yanayojirudia na mapya ili kupunguza kwa kiasi kikubwa maradhi na vifo.

16

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo jumuiya (i) za kimataifa itaendelea kuandaa na kuboresha sheria, miongozo na mikakati ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza, milipuko pamoja na yale yanayojirudia na mapya kwa wakati muafaka.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, (ii) taasisi zinazotoa huduma bila faida itahakikisha upatikanaji wa; chanjo, dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya kutosha kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya milipuko.

Serikali itashirikisha jamii na wadau wengine katika kuimarisha na (iii) kuboresha mfumo wa utoaji huduma za kinga ikiwa ni pamoja na; programu maalumu na mbinu za kuleta matokeo yanayotarajiwa katika kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, (iv) taasisi zinazotoa huduma bila faida itaendelea; kusimamia, kufuatilia, kuweka takwimu sahihi zonazotosheleza na kuratibu matokeo ya tafiti na matumizi yake kuhusu magonjwa ya kuambukiza na milipuko yanayojirudia na mapya.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, (v) taasisi zinazotoa huduma bila faida, itaimarisha uwezo kwa watumishi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza, milipuko na utayari wa kukabiliana na maafa yatokanayo na milipuko.

5.3.3 Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ajali

(a) Maelezo

Mwenendo wa magonjwa sugu au yasiyo ya kuambukiza na majeraha yanayosababishwa na ajali mbalimbali unaongezeka kwa kasi. Magonjwa ni; kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa yatokanayo na lishe duni, saratani, magonjwa ya akili na ajali zinazosababishwa na sumu mbalimbali, kujinyonga, ajali kazini na vyombo vya usafiri, mafuriko na tetemeko.

Juhudi mbalimbali zimechukuliwa na Serikali katika kukabiliana na hali hii, kwa mfano; kumarisha utambuzi wa vituo vya tiba, kutoa elimu kwa wataalam, kuimarisha mpango wa kukabiliana na majanga pamoja na kuelimisha jamii juu

17

ya udhibiti magonjwa, majanga na hali zonazojitokeza. Hata hivyo, mafanikio bado yamekuwa hafifu kutokana na upungufu wa miundombinu na gharama kubwa zinazohitajika katika kukabili hali hiyo.

(b) Madhumuni

Kubuni, kuboresha na kuimarisha mbinu mbalimbali za kubadilisha tabia na maisha potofu kwa watu na jamii, ili kuzuia na kudhibiti magonjwa sugu na yasiyo ya kuambukiza na majeraha na kupunguza athari zinazosababishwa na ajali mbalimbali.

(c) Tamko la sera

Serikali itaandaa miongozo na mikakati ya kushirikisha jamii katika (i) kudhibiti magonjwa sugu na yasiyo ya kuambukiza.

Serikali itaimarisha ushiriki wa sekta mbalimbali za umma na za (ii) binafsi katika kukabiliana na vyanzo vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ajali.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, (iii) taasisi zinazotoa huduma bila faida itaendelea; kuandaa na kurekebisha sheria, kanuni na taratibu zitakazoimarisha uzuiaji na udhibiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na ajali.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, (iv) taasisi zinazotoa huduma bila faida itaendelea; kusimamia na kuratibu tafiti kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ajali.

Kwa kushirikiana na asasi mbalimbali, Serikali itaimarisha mfumo wa (v) usafirishaji majeruhi ili kuzuia athari zinazotokana na ajali.

5.3.4 Afya ya Mama na Mtoto

(a) Maelezo

Afya ya mama na mtoto ni mfumo wa utoaji huduma maalum kwa wanawake walio katika umri wa uzazi na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, hasa watoto wachanga tangu kuzaliwa hadi siku 28. Huduma hizi zinajumuisha kutambua vidokezo hatari kwa wanawake na watoto, chanjo, tiba, elimu ya uzazi, uzazi salama, mbinu shirikishi za udhibiti wa magonjwa ya watoto, afya katika jamii, lishe na afya shuleni.

Juhudi kubwa zimefanyika na Serikali kwa kushirikiana na wananchi na

18

wadau mbalimbali katika kupanua, kuboresha na kusambaza huduma hizo kwa walengwa. Aidha, huduma za chanjo na mnyororo baridi zimeonyesha mafanikio makubwa na kuifanya nchi yetu kupata medali ya kimataifa na kuwa mfano wa kuigwa katika bara la Afrika.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, bado vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga vimeendelea kuwa juu. Kiwango cha vifo vya wanawake kimeongezeka kutoka 529 mwaka 1996 hadi kufikia 578 mwaka 2005 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai.

Kutokana na hali hiyo upo umuhimu wa kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma hii ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga kwa kiasi kikubwa.

(b) Madhumuni

Kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo na athari za magonjwa kwa wanawake wajawazito, pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka mitano hasa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kulingana na Malengo ya Milenia.

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inayotoa huduma bila faida, (i) na mashirika ya kimataifa, itaendelea kutoa huduma bila malipo kwa; wanawake wajawazito, watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa na kusimamia utekelezaji (ii) wa miongozo, mikakati na mipango endelevu ya kupunguza vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hasa watoto wachanga.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi itaboresha (iii) miundo mbinu ili kuwawezesha; wanawake wajawazito na watoto wachanga kufikiwa na kutumia huduma za afya.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuhamasisha (iv) na kuelimisha wananchi hasa wanawake kuhusu umuhimu wa huduma za afya.

19

5.3.5 Afya ya Uzazi

(a) Maelezo

Afya ya uzazi ni huduma inayotolewa kwa wanawake, wanaume na vijana walio katika umri wa kuzaa. Huduma hii inajumuisha magonjwa ya uzazi yanayohusisha; kupanga uzazi, ujauzito, magonjwa ya kujamiiana, ukeketaji na mila potofu, saratani ya via vya uzazi, kuzuia na kutibu ugumba. Huduma ya afya ya uzazi imeendelea kuboreshwa nchi nzima kwa kiwango cha kuridhisha. Makundi mbalimbali yanashiriki katika kupata huduma hizi katika vituo vya kutolea huduma.

Hata hivyo, kutokuwepo kwa elimu na uhamasishaji wa kutosha wa afya ya uzazi kwa makundi mbalimbali na hasa vijana na wanaume kumesababisha kuongezeka kwa magonjwa ya ngono pamoja na matatizo ya mimba zisizotarajiwa, hasa maeneo ya vijijini. Pia, mila potofu zimechangia katika kuzorotesha afya ya uzazi katika baadhi ya maeneo.

(b) Madhumuni

Kuboresha huduma ya afya ya uzazi kwa makundi yote na hasa; wanaume, vijana na watu wenye ulemavu ambao wamekuwa hawashiriki kikamilifu.

(c) Tamko la sera

Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali kuimarisha afya ya uzazi (i) ya wanawake na wanaume, watu wenye ulemavu, vijana na wazee.

Serikali itaandaa miongozo, mikakati na kuratibu shughuli zinazolenga (ii) afya ya uzazi ya makundi mbalimbali pamoja na kuhakikisha huduma za uzazi wa mpango unatekelezwa.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha utoaji (iii) wa huduma bora za uzazi katika vituo vya kutolea huduma za afya zinazowavutia wanawake, wanaume na vijana.

5.4 Tiba

Maelezo (a)

Serikali ina jukumu la kusimamia huduma za afya nchini katika vituo vya umma, mashirika ya dini, mashirika yasio ya kiserikali na watu binafsi. Aidha, tiba inatakiwa kuwa salama kulingana na mahitaji ya wagonjwa na kwa uwiano. Ili kufikia azma hii, kila ngazi inatakiwa kuwa na wataalam, majengo na vifaa kulingana na mwongozo wa majukumu ya ngazi husika. Vilevile, wagonjwa

20

wanatakiwa kupata rufaa kutoka ngazi moja kwenda nyingine kulingana na matatizo na uwezo wa kituo cha huduma za afya.

Hali halisi ni kwamba huduma za tiba, utengamao na mfumo wa rufaa hazitoshelezi mahitaji ya wagonjwa katika ngazi zote za utoaji huduma. Hali hii imesababisha malalamiko kutoka kwa wananchi na wagonjwa wengi kulazimika kupata rufaa nje ya nchi kutokana na ukosefu wa wataalam na vifaa nchini.

Madhumuni(b)

Kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya, utaratibu wa rufaa, upatikanaji wa wataalam na vifaa ili kuboresha huduma za afya zilizo sahihi, salama, uwiano na endelevu.

Tamko la sera(c)

Serikali itasimamia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya mfumo, (i) muundo na rufaa ya utoaji tiba kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya hadi hospitali za ngazi mbalimbali.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa kila kijiji kina (ii) zahanati na kila kata ina kituo cha afya ili kuleta uwiano katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa rufaa (iii) nchini ili kuboresha matumizi ya wataalam na raslimali kwa lengo la kupunguza idadi, aina na gharama za kutibu wagonjwa nje ya nchi.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha huduma za tiba ngazi (iv) ya kaya kwa magonjwa sugu na yenye kuhitaji matibabu ya muda mrefu.

Serikali kwa kushirikiana na wamiliki wa vituo vya kutolea huduma (v) za afya itaimarisha usimamizi unaofanywa na Bodi na Kamati katika ngazi mbalimbali.

Serikali itaweka mazingira mazuri ya kushirikisha jamii kuimarisha (vi) huduma za utambuzi wa awali na utengamao unaosababishwa na magonjwa mbalimbali na ajali.

21

5.4.1 Mfumo wa utoaji huduma za afya kwa uwiano wa kijiografia

(a) Maelezo

Ni mfumo wa rufaa unaotoa huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati , vituo vya afya na hospitali ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma za afya karibu na eneo analoishi. Katika mfumo huu, zahanati zilipangwa kujengwa umbali wa kilometa 5 za mduara na kilometa 10 za mduara kwa kila kituo cha afya, hospitali katika kila wilaya, mkoa na pia hospitali za rufaa na maalum.

Mafanikio ya utaratibu huu, ni kuwa na idadi kubwa ya zahanati, vituo vya afya, hospitali maalum na hospitali za rufaa zenye mpangilio mzuri wa kutoka ngazi ya kijiji hadi ngazi ya Taifa. Hata hivyo, kutokana na nchi yetu kuwa kubwa, kuongezeka kwa idadi ya watu, upungufu mkubwa wa wafanyakazi na vitendea kazi, ufinyu wa bajeti, umbali mrefu wa kufikia huduma za afya umesababisha lengo la kuongeza uwiano wa upatikanaji wa huduma za afya lisifikiwe kama ilivyotarajiwa. Juhudi zitaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi.

Madhumuni(a)

Kuwa na mfumo madhubuti na endelevu wa utoaji huduma, unaozingatia uwiano na usawa katika upatikanaji wa huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi wananchi wote.

Tamko la sera(b)

Serikali itaendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa (i) kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata na hospitali kwa kila wilaya, hospitali ya rufaa kila mkoa na hospitali maalum ngazi ya taifa kwa kushirikiana na wananchi na wadau wote kwa ujumla.

Serikali itaandaa na kupitia miongozo inayosimamia mfumo wa utoaji (ii) wa huduma za afya kwa uwiano kwa kuzingatia mahitaji ya makundi maalum.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itaweka utaratibu (iii) utakaowezesha kupatikana kwa watumishi wa kutosha na wenye ujuzi unaotakiwa.

Serikali itaimarisha huduma za rufaa nchini kwa kupandisha ngazi (iv)

22

hospitali za mkoa kuwa daraja la pili za rufaa na hospitali za wilaya kuwa daraja la kwanza.

Serikali itasimamia upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, samani (v) pamoja na mitambo husika katika vituo vya kutolea huduma za afya .

Serikali itaweka na kusimamia viwango kwa majengo yote ya kutolea (vi) huduma za afya na kuimarisha utaratibu wa mahusiano na watoa huduma wote.

Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi itaendeleza juhudi (vii) zake za kupanua na kukarabati majengo ya kutolea huduma za afya.

Serikali itahakikisha kuna uwiano kijiografia katika kutoa huduma za (viii) afya hapa nchini.

5.4.2 Uuguzi na Ukunga

(a) Maelezo

Huduma za uuguzi na ukunga zinatolewa katika mfumo uliopo kwenye ngazi mbalimbali za huduma za afya nchini. Uuguzi na ukunga ni muhimu katika kupunguza maumivu kwa wagonjwa, kuboresha huduma za mama na mtoto na makundi mengine ya jamii.

Huduma za uuguzi na ukunga zimezoeleka kwamba zinatolewa katika mazingira ya zahanati, vituo vya afya na hospitali tu za umma na binafsi. Hali halisi ni kuwa huduma hizo sasa zinatolewa pia nje ya vituo hivyo katika kaya na jamii. Hali hii imetokana na kuwepo kwa ongezeko la magonjwa sugu yanayohitaji tiba na matunzo ya muda mrefu, mahitaji ya huduma za utengemao na umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika upangaji na utoaji wa huduma za afya.

Hivyo, wigo na ubora wa huduma za uuguzi na ukunga unahitaji kuinuliwa ili kukidhi matarajio ya wananchi, uwiano, viwango, usalama.

(b) Madhumuni

Kuimarisha ubora na usalama wa huduma za uuguzi na ukunga nchini kwa kuzingatia masharti na viwango vya huduma bora na mahitaji ya wananchi.

23

(c) Tamko la Sera

(i) Serikali kwa kushirikiana na wadau itaboresha mazingira ya utoaji wa huduma za uuguzi na ukunga katika sekta za umma na binafsi.

(ii) Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha huduma za utengamao kuanzia katika vituo vya huduma hadi katika kaya na jamii.

5.4.3 Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi

Maelezo(a)

Upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi ni muhimu katika utoaji wa huduma za afya. Aidha, upatikanaji wake ni moja ya vivutio kwa wananchi kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Pamoja na jitihada za Serikali za kuhakikisha kwamba, dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vinapatikana, bado kuna upungufu na matatizo ya upatikanaji wake katika vituo vya kutolea huduma za afya na hivyo kuathiri utoaji wa huduma bora.

Madhumuni(b)

Kuhakikisha kwamba dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vinapatikana wakati wote, kwa kiasi cha kutosha na ubora unaotakiwa.

Tamko la sera(c)

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa upatikanaji (i) wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya nchi.

Watengenezaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi watawekewa (ii) mazingira mazuri ya uzalishaji hapa nchini.

Mfumo wa matunzo na matengenezo ya vifaa vya kutolea huduma za (iii) afya utaimarishwa.

Serikali itaendelea kuimarisha utengenezaji na upatikanaji wa vifaa (iv) vya utengemao na kwa bei nafuu.

24

5.4.4 Uchunguzi wa magonjwa kwa njia ya maabara na radiolojia

(a) Maelezo

Uchunguzi wa magonjwa ni kiungo muhimu katika utoaji wa huduma za kinga, tiba na utengemao. Hivyo, uimarishaji wa uchunguzi wa magonjwa ni moja ya nguzo muhimu katika utoaji wa huduma za afya. Hata hivyo, pamoja na juhudi za Serikali kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa na vyanzo vya vifo kutokana na makosa ya jinai au mauaji bado hazijafikia kiwango cha kuridhisha na hivyo zinahitaji kuimarishwa.

(b) Madhumuni

Kuwa na huduma bora na za kisasa za uchunguzi wa magonjwa na vyazo vya vifo.

(c) Tamko lo Sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha huduma za uchunguzi (i) wa magonjwa na vyanzo vya vifo.

Serikali itaimarisha uhakiki wa huduma za uchunguzi wa magonjwa na (ii) vifo.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha upatikanaji wa vifaa (iii) vya maabara, radiolojía na vitendanishi.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa matengenezo (iv) na huduma kinga ya vifaa vya maabara na radiología.

5.4.5 Afya ya Kinywa

Maelezo(a)

Afya ya kinywa ni sehemu muhimu katika afya ya jamii. Watanzania wengi wana magonjwa na matatizo mbalimbali katika vinywa vyao. Magonjwa ya kinywa yaliyo mengi yanaweza kuzuilika kwa kuzingatia taratibu za afya. Aidha, magonjwa ya meno yameongezeka kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha na vyakula. Magonjwa ya Saratani, UKIMWI na maji yenye madini ya florini yanaathiri afya ya kinywa ya wananchi walio wengi.

Hivi sasa, Serikali inatoa huduma za afya ya kinywa kwa wananchi ngazi za wilaya, mkoa na taifa. Hata hivyo, huduma hizi hazijawafikia wananchi walio wengi hususan wanaoishi vijijini. Aidha, huduma zinazotolewa za sasa

25

hazikidhi mahitaji kutokana na mabadiliko ya teknolojia ya afya ya kinywa.

Madhumuni(b)

Kuwa na huduma za afya ya kinywa zilizo bora na za kisasa zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

Tamko la Sera(c)

Serikali itaandaa kanuni, miongozo na taratibu za utoaji huduma za (i) afya ya kinywa.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itapanua huduma za afya ya (i) kinywa sanjari na huduma nyingine za afya.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha, kuendeleza na (ii) kuratibu tafiti za magonjwa ya kinywa.

Serikali ikishirikiana na wadau itaendelea kuwaelimisha wananchi juu (iii) ya afya ya kinywa.

5.4.6 Damu salama

(a) Maelezo

Mfumo wa damu salama unaotumika kwa sasa nchini ni ule wa kila hospitali kuwa na utaratibu wake wa kukusanya, kupima na kutumia damu. Aidha, mfumo huu unategemea zaidi ukusanyaji wa damu kutoka kwa ndugu wa wagonjwa kuliko kwa watoa damu wa kujitolea kwa hiari. Mfumo huu unasababisha kuwepo kwa uhaba wa damu na uwezekano wa maambukizo ya magonjwa yanayotokana na kuongezewa damu yenye matatizo au ugonjwa kama vile; UKIMWI, Kaswende, Homa ya Ini “Hepatitis B na Hepatitis C”.

(b) Madhumuni

Kuimarisha mfumo wa kitaifa ambao unasimamia ukusanyaji, upimaji, utunzaji, usambazaji na matumizi ya damu salama nchini.

(c) Tamko la sera

Serikali itaandaa na kusimamia sheria, kanuni, miongozo na taratibu (i) za upatikanaji na matumizi ya damu salama.

Serikali itaboresha mazingira kwa wananchi, kuwawezesha kutoa (ii) damu kwa hiari.

26

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha miundombinu ya (iii) upatikanaji, utunzaji na usambazaji wa damu salama.

Wananchi watahamasishwa, ili kuchangia huduma za upatikanaji wa (iv) damu salama.

5.4.7 Dawa za Kulevya na Afya ya Akili

(a) Maelezo

Afya ya akili ni sehemu muhimu ya huduma za afya ya jamii. Magonjwa na ulemavu wa akili vimekuwa vikiongezeka katika jamii kutokana na mabadiliko ya hali ya maisha na pia kuporomoka kwa mila na desturi nzuri ambazo ni muhimili na nyenzo za kinga dhidi ya magonjwa ya akili. Taratibu za jadi za kinga dhidi ya ulevi wa pombe wa kupindukia na matumizi ya dawa za kulevya zimelegalega katika jamii.

Huduma za afya ya akili nchini ni duni, kutokana na kutopewa umuhimu wake na upungufu wa wataalam wa magonjwa ya akili. Aidha, hakuna takwimu sahihi za hali halisi ya magonjwa ya akili na wenye ulemavu wa akili nchini. Vile vile, suala la unyanyapaa limeathiri upatikanaji wa huduma bora za afya ya akili.

(b) Madhumuni

Kupanua na kuimarisha wigo na ubora wa huduma za afya ya akili.

(c) Tamko la sera

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa huduma za (i) kinga, tiba na utengamao wa matumizi ya dawa za kulevya na athari zake.

Serikali itapitia na kuboresha sheria, kanuni, miongozo na taratibu za (ii) kutoa huduma kwa wagonjwa wa akili, kwa kuzingatia utu na haki.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, itahakikisha kuwa (iii) huduma za afya ya akili zinawafikia wananchi wengi kulingana na mahitaji.

Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha mfumo wa utoaji (iv) huduma na usimamizi wa huduma za afya ya akili nchini.

27

(v) Jamii itashirikishwa katika kuboresha utoaji wa huduma za afya ya akili.

(vi) Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa huduma za kinga dhidi ya dawa za kulevya, tiba na utengamao wa waathirika wa pombe na dawa za kulevya.

5.4.8 Ushirikishaji, Uchangiaji na Msamaha wa Huduma za Afya

5.4.8.1 Ushiriki wa jamii katika upatikanaji huduma za afya

(a) Maelezo

Wananchi wamekuwa wakishiriki kwa hali na mali katika upatikanaji wa huduma za afya kwa kujenga, kukarabati na kutunza vituo vya huduma za afya. Aidha, wanashiriki katika uendeshaji kupitia bodi na kamati zao. Hata hivyo, ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika upatikanaji na usimamizi wa huduma za afya bado uko chini.

(b) Madhumuni

Kuendeleza ushirikishaji wa jamii katika maamuzi ya upatikanaji, utoaji, uendeshaji na umiliki wa huduma za afya.

Tamko la sera(d)

Serikali itakamilisha uundwaji wa Bodi na kamati za huduma za afya, (i) katika ngazi mbalimbali na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yao.

(ii) Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itahamasisha na kuweka mazingira mazuri, kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika upatikanaji wa huduma za afya, ikiwa ni pamoja na; ujenzi, ukarabati, upangaji, uendeshaji na utumiaji wa vituo vya kutolea huduma.

5.4.8.2 Uchangiaji wa gharama za huduma za afya

(a) Maelezo

Kutokana na athari za kuyumba kwa uchumi katika miaka ya 1980, gharama za utoaji wa huduma zimepanda. Aidha, ufinyu wa bajeti ya Serikali na ongezeko la watu vimesababisha bajeti ya Serikali na hasa ile ya sekta ya afya kuwa tegemezi kwa wahisani. Hii imefanya huduma hizi kutokuwa endelevu

28

na wananchi wenyewe kutoshiriki kuzimiliki kikamilifu. Kwa hali hii, katika mwaka 1993, Serikali iliamua kushirikisha wananchi katika kuchangia gharama za huduma za afya kupitia sera ya uchangiaji gharama. Pamoja na kuwepo kwa sera hii, bado uchangiaji hauridhishi na hivyo unatakiwa kuimarishwa.

(b) Madhumuni

Kupanua uwigo, kuimarisha na kuendeleza vyanzo vya mapato vya kuendeshea huduma za afya kwa nia ya kuboresha huduma na kupunguza utegemezi na kuimarisha ushiriki na umiliki wa huduma hizi kwa wananchi.

(c) Tamko la sera

Serikali itaboresha na kuendelea kusimamia mikakati na miongozo (i) ya uchangiaji wa gharama za huduma za afya pamoja na matumizi ya mapato yanayotokana na uchangiaji huo.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kubuni njia endelevu (ii) za kuchangia gharama za huduma za afya kwa manufaa ya wananchi wote kama vile Bima za Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii.

Msamaha wa uchangiaji gharama huduma za afya kwa makundi maalum1.1.1.3

(a) Maelezo

Serikali inatambua kuwepo kwa wananchi wasio na uwezo wa kuchangia gharama za huduma za afya, ikiwa ni pamoja na wale walio katika makundi maalum ya kijamii, mathalani; wazee walio na umri zaidi ya miaka 60 ambao hawana uwezo wa kipato, watoto wenye umri chini ya miaka mitano, watoto walio katika mazingira hatarishi, wanawake wajawazito na watu wasiojiweza kiuchumi. Pia, wenye magonjwa sugu kama; saratani, UKIMWI, kisukari, magonjwa ya moyo, pumu, sickle cell, kifua kikuu, ukoma na magonjwa ya akili.

(b) Madhumuni

Kuwezesha makundi maalum kupata huduma bora za afya sawa na wananchi wengine.

29

(c) Tamko la sera

Serikali itaboresha, itaandaa na kusimamia sheria, kanuni na miongozo (i) ya uchangiaji gharama za huduma za afya ikiwemo msamaha kwa makundi maalum.

Serikali itahakikisha kuna uwiano katika kutoa huduma za afya kwa (ii) makundi yote.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa utaratibu mzuri wa (iii) namna ya kuyahudumia makundi maalum yanayostahili msamaha.

5.4.9 Ushirikishaji wa mashirika ya dini, asasi zisizo za kiserikali na sekta binafsi

(a) Maelezo

Serikali inatambua umuhimu wa mchango wa wadau toka sekta binafsi, mashirika ya dini na asasi zisizo za kiserikali katika utoaji wa huduma za afya. Hata hivyo, kuna udhaifu katika ushiriki na ushirikishwaji wa wadau wa sekta hiyo.

(b) Madhumuni

Kuboresha ushiriki wa mashirika ya dini na sekta binafsi ili kupanua uwigo wa kutoa huduma za afya na kuleta uwiano zaidi katika upatikanaji wake.

(c) Tamko la sera

Serikali itaendelea kushirikisha mashirika ya dini na sekta binafsi (i) katika utoaji wa huduma za afya kwa kutumia mikataba, makubaliano maalum na miongozo mbalimbali.

Serikali itaendelea kutambua na kushirikiana na mashirika ya dini na (ii) asasi mbalimbali zisizo za kiserikali katika kutoa huduma za afya na kulinda haki za makundi maalum.

Serikali itaweka na kusimamia viwango vya utoaji wa huduma za afya (iii) katika ngazi zote.

30

5.4.10 Huduma za afya binafsi

Maelezo(a)

Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi, mashirika ya dini na asasi za hiari au zisizokuwa za kiserikali katika kupanua wigo wa utoaji wa huduma za afya nchini. Uanzishwaji wa huduma za afya binafsi umeongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, Serikali imeruhusu watumishi wa umma kutoa huduma za afya binafsi baada ya saa za kazi.

Mchango wa sekta binafsi umesaidia juhudi za Serikali katika kufikisha huduma za afya kwa wananchi, hasa pasipo na vituo vya umma. Hata hivyo, ongezeko la vituo binafsi limesababisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya wataalam wa afya kukidhi sekta za umma na binafsi. Hali hii imesababisha baadhi ya watumishi katika vituo vya umma kwenda kutoa huduma katika vituo vya afya binafsi.

Hata hivyo, imebainika kwamba baadhi ya watumishi wa umma hutumia muda wa saa za kazi kutoa huduma katika vituo vyao binafsi. Pamoja na nia njema ya Serikali, hali hii imesababisha malalamiko kwa watumiaji wa huduma katika vituo vya umma.

Madhumuni(b)

Kuweka mfumo madhubuti wa kusimamia huduma za afya zinazotolewa na watu binafsi, watumishi wa umma, mashirika ya dini na mashirika ya hiari au yasiyokuwa ya kiserikali.

Tamko la sera(c)

Serikali itaimarisha utoaji wa huduma za afya za watu binafsi, (i) watumishi wa umma, mashirika ya dini na mashirika ya hiari au yasiyokuwa ya kiserikali.

Serikali itatoa mwongozo wa watumishi wa umma kuhusu utoaji (ii) wa huduma za kitaalamu katika vituo vya kutolea huduma vya watu binafsi kulingana na sheria, kanuni na taratibu.

31

5.4.11 Tiba Asilia, Tiba Mbadala na Ukunga wa Jadi

(a) Maelezo

Tiba asilia inatumiwa na wananchi wengi. Takribani asilimia sitini ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa na maradhi kabla ya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, hivi karibuni tiba mbadala imepata umaarufu miongoni mwa wananchi kutokana na uimarikaji wake duniani.

Kadhalika, wagonjwa hutoka hospitalini na kwenda kutafuta tiba asilia au kutumia aina zote za tiba kwa pamoja. Vilele, takwimu zinaonyesha kwamba bado kuna wanawake wajawazito wanaojifungulia nyumbani kwa kusaidiwa na wakunga wa jadi. Pamoja na huduma hizi kutumiwa na wananchi wengi, uratibu wa uendeshaji wake unahitaji kuimarishwa.

(b) Madhumuni

Kuendeleza, kuratibu na kuboresha utoaji wa huduma za tiba asilia, mbadala na ukunga wa jadi.

(c) Tamko la sera

Serikali itaandaa kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi wa utoaji (i) huduma za tiba asilia, tiba mbadala na ukunga wa jadi.

Watoa huduma za tiba asilia, tiba mbadala na ukunga wa jadi (ii) watashirikishwa kuboresha na kusimamia utoaji wa huduma hizo.

Wadau watashirikishwa katika kuweka mfumo madhubuti wa kulinda (iii) mazingira na mimea inayotumika katika tiba asilia na tiba mbadala.

Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha, kuendeleza na (iv) kuratibu tafiti za tiba asilia, tiba mbadala na ukunga wa jadi.

5.5 Huduma za Utengemao

(a) Maelezo

Inajumuisha juhudi mbalimbali zinazofanywa ili kumwezesha mtu mwenye ulemavu kuona kuwa ulemavu sio kikwazo cha maendeleo yake na kuwa anaweza kuvitumia viungo alivyonavyo kujiendeleza, katika nyanja mbalimbali kama watu wengine. Huduma hizi, ziko katika nyanja za kijamii na kitabibu.

32

Juhudi hizi ni pamoja na kutoa ushauri nasaha kwa mhusika ili aikubali hali yake na kumshauri kuhusu kazi anazoweza kuzifanya zikamnufaisha yeye na taifa kwa ujumla.

Aidha, kuishauri familia yake na jamii inayomzunguka kumhamasisha kujiendeleza ili aweze kujitegemea. Juhudi zinaendelea kumsaidia mwathirika kupewa mazoezi ya viungo kuimarisha viungo vilivyoko, mazoezi ya kiakili ya kuamsha upya hali ya ubongo na ku