Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 07Article 517517

Siasa of Monday, 7 December 2020

Chanzo: Millard Ayo

ACT Wazalendo yakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

ACT Wazalendo yakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo imeielekeza Kamati ya Uongozi ya chama hicho kupendekeza jina la mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Aidha, Kamati hiyo imeazimia kuwaruhusu Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wa chama hicho waliochaguliwa kwenda kukiwakilisha na wananchi waliowachagua.

Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 6, na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu wakati akitoa maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Join our Newsletter