Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 30Article 516668

Siasa of Monday, 30 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Aliyeshinda uenyekiti Mpwapwa aahidi makubwa

Aliyeshinda uenyekiti Mpwapwa aahidi makubwa

MSHINDI wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime ameahidi kuongeza mapato katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano.

Akizungumza baada kutangazwa kuwa mshindi, Fuime alisema: "Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo nitajitahidi kuboresha mapato ya halmashauri na kushughulikia changamoto za

Fuime pia alisema halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri kongwe nchini kwa kushirikiana na watalaamu atahakikisha anaongeza vyanzo vya mapato na kusimamia mapato ili yaweze kuleta mabadiliko katika miradi ya maendeleo.

Fuime ni diwani Mteule wa Kata ya Mpwapwa Mjini aliibuka kidedea katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kuwashinda wapinzani wake Kayanda Mwanika na Baraka Habari.

Katika uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, uliosimamiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Mpwapwa, Jackson Shiluah na kumwibua Fuime kuwa mshindi kati ya wagombea watatu kwa kupata kura 31, Kayanda Mwanika kura 13 na kura moja iliharibika na Baraka Habari alipata kura 0.

Hivyo Shiluah alimtangaza Huime kuwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano katika uchaguzi uliohusisha nafasi mbili ya mwenyekiti wa halmashauri na

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Diwani Mteule wa Kata ya Luhudwa Richard Maponda naye alishinda katika kinyang'anyiro hicho kwa kupata kura 36 kati ya 45 zilizopigwa ambapo mpinzani wake, Octan Bahatisha alipata kura 09.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Richard Maponda alisema watajitahidi kusimamia kwa kina sekta zinazo jumuisha kundi kubwa la wananchi ambalo ni walima na wafugaji.

Mmoja wa wananchi wa wilaya hiyo ambaye amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Mlunduzi na Katibu Mwenezi wa CCM wilayani, Mazengo John alisema, sasa ni wakati wa madiwani kuunganisha nguvu za pamoja iliekuweza kuwahudumia wapiga kura wao bila kujali majimbo wanayotoka.

"Natambua uchaguzi wote haukosi kuacha makovu kwa wagombea au wafuasi wao. Mimi ninachoweza kusema kuwa lazima madiwani na wabunge kuanza kazi pamoja ili kuweza kuifanya halmashauri isonge mbele kwani imechelewa sana kimaendeleo hivyo tunahitaji kasi kubwa kuwafikia malengo yetu,"alisema John.

Halmashauri ya Mpwapwa yenye kata 33 ambazo zote huongozwa na CCM ambapo kati ya madiwani hao 33 wa kata 21 na madiwani 12 ni wa viti maluumu. Madiwani wapya ni 20 na waliokuwapo katika baraza la madiwani lililopita ni 13.

Join our Newsletter