Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 10 31Article 513460

Siasa of Saturday, 31 October 2020

Chanzo: HabariLeo

CCM Z’bar yazoa majimbo 46, wapinzani 6

CCM Z’bar yazoa majimbo 46, wapinzani 6

MATOKEO ya ubunge katika majimbo 52 ya Zanzibar yanaonesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika majimbo 46.

Majimbo manne ya ubunge yamechukuliwa chama cha ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (CUF) kimepata majimbo mawili.

Ofisa wa uchaguzi wilaya ya Chake Chake Pemba, Maulid Mwalimu alisema CUF kimeibuka na ushindi wa nafasi za ubunge katika majimbo ya Mtambile pamoja na Pandani Wete Pemba.

Mgombea Seif Salim Seif wa CUF aliibuka na ushindi wa jimbo la Mtambile kwa kupata kura 2,258 huku nafasi ya uwakilishi ikishikiliwa na mgombea kutoka CCM, Mohamed Mgaza Jecha aliyepata kura 3,0534.

Chama cha ACT-Wazalendo kimeibuka na ushindi katika majimbo manne ya Pemba ambayo ni Gando,Wete,Kojani pamoja na Mtambwe ambalo mgombea wake Habib Ali Mohamed ameibuka na ushindi.

Kwa upande wa Unguja, CCM kumeibuka na ushindi katika jimbo la Bumbwini kwa kupata kura 9,632 kwa upande wa ubunge kupitia mgombea wake Mbarouk Yussuf ambaye mwaka 2015 alipoteza jimbo hilo na kuchukuliwa na wapinzani.

''Namshukuru Mungu kwa muda wa miaka mitano sikununa nilifanya kazi na wananchi bega kwa bega kutafuta maendeleo ya wananchi''alisema Yussuf.

CCM kimefanikiwa kuchukua majimbo ya ubunge 12 katika kisiwa cha Pemba chenye majimbo 18 hiyo ikiwa ni rekodi kwa mara ya kwanza kufanya vizuri tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.

Join our Newsletter