Uko hapa: NyumbaniHabariSiasa2021 10 11Article 562636

Siasa of Monday, 11 October 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

CHADEMA tupo tayari kuzungumza na Rais

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara

"Mwezi April Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Samia ya kuhitaji kukutana naye, Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ila kundi la Wanasiasa bado, tuna imani ya kukutana naye tumweleze mambo yanayosababisha ufa kwenye Taifa hili"

"Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili"

"Baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu katiba mpya, tulimwandikia Rais Mstaafu Kikwete barua ya hitaji hilo akakubali kukutana nasi, tukashauriana na mchakato uliishia ulipoishia, alipoingia Rais Magufuli tuliandika barua nne na zote hazikujibiwa"

"Moja ya kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuwasemea watu ambao hawana majukwaa ya kusemea mfano ni machinga na wengine, unapozuia mikutano ya vyama vya siasa maana yake umezua majukwaa ya Watu hao wasiseme na wasiwe na sauti za kusema"——— Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara