Uko hapa: NyumbaniHabariSiasa2021 09 07Article 555925

Siasa of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

CHADEMA wagoma kukutanishwa na jeshi la polisi

CHADEMA wakataa kukutanishwa na Polisi CHADEMA wakataa kukutanishwa na Polisi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakipo tayari kukutanishwa na jeshi la polisi, kama ambavyo ametangaza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ili kuondoa mvutano kati yao, vyama vya siasa na jeshi hilo.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Septemba, 7,2021 na Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipozungumza na waandishi wa habari.

Mrema amesema hawaoni haja ya kukutanishwa na jeshi hilo kwa kuwa kwa mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya kwa miaka sita amedai ni wahalifu ambao wangetakiwa wawe wameshafikishwa kwenye vyombo vya sheria.