Uko hapa: NyumbaniHabariSiasa2021 10 29Article 566533

Siasa of Friday, 29 October 2021

Chanzo: mwananchidigital

Chadema kutoshiriki uchaguzi Ngorongoro

Chadema kutoshiriki uchaguzi Ngorongoro Chadema kutoshiriki uchaguzi Ngorongoro

Chadema imetangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Ngorongoro huku ikionya watakaochukua fomu kwa jina la chama hicho.

Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, William Ole Nasha aliyefariki Septemba 27 jijini Dodomabaada ya kuugua kw amuda mfupi.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema msimamo wa chama hicho bado ni kutoshiriki uchaguzi hadi kufanyika mabadiliko ya tume ya uchaguzi.

"Hatuna imani na Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) na huu ndio msimamo wetu, hivyo hatutashiriki uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro, japo tunao wanachama wenye sifa ya kugombea," amesema Golugwa.

Amedai kuwapo watu walioandaliwa kwenda NEC kuchukuwa fomu, akisema: “Tutachukuwa hatua kali na tunataka jamii ijue hatutakuwa na mgombea Ngorongoro," amesema.

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015 Chadema ilipata madiwani kadhaa katika jimbo hilo lakini hata hivyo baadaye walijiuzulu na kujiunga na CCM.

Hadi Sasa chama ambacho kinaendelea na mchakato wa kugombea jimbo hilo ni CCM ambao wagombea 17 walichukuwa fomu ndani ya chama hicho na wameshiriki kura za maoni.