Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 09 25Article 510394

Siasa of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Chagueni CCM, chama chenye mipango - Majaliwa

Chagueni CCM, chama chenye mipango - Majaliwa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wananchi waichague CCM ili iweze kuwaletea maendeleo.

"Chagueni CCM, chama chenye mipango ya maendeleo na ya kueleweka. Chama chenye mipango ndani ya kitabu chenye kurasa 303. Naomba kura zenu ili tuwaletee maendeleo."

Alitoa wito huo jana jioni wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Misheni.

"Zamani tulikuwa na kitabu kidogo cha kurasa 236 lakini sasa hivi tuna buku kubwa zaidi. Tukitekeleza yote haya, mambo si yatakuwa mazuri zaidi,?" alihoji.

Join our Newsletter