Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 07Article 517538

Siasa of Monday, 7 December 2020

Chanzo: HabariLeo

Chuki zamfanya Mwenezi Chadema kutimkia CCM

Chuki zamfanya Mwenezi Chadema kutimkia CCM

ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Mpanda Mjini katika Mkoa wa Katavi, James Mwailwa, amekihama chama hiko na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema alichukua uamuzi huo kutokana na Chadema kumejaa mahubiri ya chuki, unyanyasaji, ukandamizaji na mambo yasiyofaa kidemokrasia.

Mwailwa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Jimbo la Mpanda Mjini kati ya mwaka 2015-2018, pia alikuwa Mratibu wa Uchaguzi wa Oktoba 2020 wa aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya Chadema.

Mwailwa alikabidhiwa kadi ya CCM na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Abeli Kimazi, aliyesema anawakaribisha na kuwaalika vijana wengine waliobaki Chadema na katika vyama vingine vya upinzani wenye nia ya kulitendea haki taifa hili, kujiunga na CCM.

Kimazi alimtaka Mwailwa kuendelea kuwakumbusha watu aliowaacha Chadema mambo makubwa na mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM.

Join our Newsletter