Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 09 25Article 510412

Siasa of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Dk Mabula aahidi kuboresha michezo Ilemela

Dk Mabula aahidi kuboresha michezo Ilemela

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema kuwa atahakikisha kuwa anaendelea kuboresha sekta ya michezo katika wilaya hiyo.

Akizungumza mapema leo, Dk Mabula alisema katika kipindi cha miaka mitano,Halmashauri ya Ilemela imefanikiwa kujenga viwanja vya michezo katika eneo la Sabasaba.

Hata hivyo alisema takribani zaidi ya Sh milioni 171 zimetengwa kwajili ya ujenzi wa viwanja hivyo vya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu na mpira wa Pete.

Dk Mabula alisema kupitia viwanja hivyo wameweza kuibua vipaji mbali mbali vya michezo pia na wilaya yao ilifanikiwa kufanya vyema katika mashindano ya michezo Shule ya msingi(UMITASHUMTA) na sekondari(UMISSETA).

Join our Newsletter