Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 09 25Article 510364

Siasa of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Dk Mabula aahidi ujenzi wa zahanati Ilemela

Dk Mabula aahidi ujenzi wa zahanati Ilemela

MGOMBEA wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula ameahidi kuwajengea wakazi wa kata ya Ilemela zahanati iwapo watampa dhamana ya kuliwakilisha jimbo hilo bungeni.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika shule ya msingi Ilemela,Dk Mabula alisema atajenga zahanati hiyo pamoja na kuboresha kituo cha Afya cha Lumala ambapo tayari Serikali imetenga Sh milioni 60 kwajili ya maboresho hayo.

Aliahidi katika zahanati itakayojengwa ataweka jengo la mama na mtoto.

Kuhusu miundo mbinu ya barabara, Dk Mabula alisema Halmashauri imetenga Sh milioni 151 kwajili ya ujenzi wa barabara za Ilemela-Mahakamani, Majengo mapya-Lumala, Pasiansi-Kiseke.

Katika Elimu,Dk Mabula alisema wametenga Sh milioni 44 kwajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 10 katika shule ya sekondari Lumala pamoja na shule ya msingi Mwambani.

Naye Mgombea udiwani kupitia CCM, Wilbard Kilenzi alisema katika sekta ya ardhi kwenye kata yao jumla ya viwanja 1260 vimepimwa na Serikali ilitoa bilion3 na milioni 30 kwajili ya kumaliza kero ya mgogoro wa ardhi katika eneo la Nyakuguru. Alisema serikali ilifanikisha katika utatuzi wa mgogoro wa makaburi baina ya wakristo na waislamu katika eneo la Lumala.

Aidha alisema kupitia juhudi za Mbunge Mabula na Serikali wamefanikisha kujenga madarasa matatu katika shule ya msingi Jeshini na Mwambani. Pia walijenga darasa moja katika shule ya msingi Sabasaba.

Join our Newsletter