Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 26Article 516191

Siasa of Thursday, 26 November 2020

Chanzo: Millard Ayo

"Ile Ofisi ni mali ya Jiji, labda ile ndogo anataka kubwa" Sugu

"Ile Ofisi ni mali ya Jiji, labda ile ndogo anataka kubwa" Sugu

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi, amesema yeye hana mamlaka ya kumkabidhi ofisi mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia CCM Dkt. Tulia Ackson, kwani ofisi aliyokuwa akiitumia, alikwisharudisha funguo kwa mamlaka husika na kwamba amuache na achape kazi

“Wewe umeshasikia wapi mbunge analia hajakabidhiwa ofisi, hakuna kitu kama hicho, aliyempa cheti cha ubunge ndiye angemwelekeza kwamba kinachofuata ni nini, afanye kazi aachane na Sugu” Sugu

“Yeye afuate utaratibu pengine hata sasa wamempa ofisi nyingine yeye ni mtu wa kujimwambafai, labda ofisi niliyokuwa naitumia mimi ni ndogo nadhani haitaki anatafuta ‘justification’ wampe ofisi kubwa zaidi kwa kusema Sugu hajanikabidhi ofisi, ofisi ni mali ya jiji” Sugu

BREAKING: DIEGO MARADONA AFARIKI DUNIA

Join our Newsletter