Uko hapa: NyumbaniHabariSiasa2021 09 14Article 557383

Siasa of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kauli ya Dr. Ndugulile baada ya uteuzi wake kutenguliwa

Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni

Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuwa waziri.

Rais Samia alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kutengua uteuzi wa mawaziri watatu akiwamo Ndugulile na kuteua wapya wanne ambao ni Dk Ashatu Kijaji, Dk Stergomena Tax, January Makamba na Profesa Makame Mbarawa.

Ndugulile uteuzi wake ulienguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Kijaji ambaye ni mbunge wa Kondoa Vijijini.

Ndugulile ameandika hayo jana Jumatatu Septemba 13, 2021 kupitia mtandao wa kijamii amewashukuru wadau wa Tehama kwa ushirikiano waliompa na ametoa pongezi kwa Kijaji kuteuliwa.