Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 24Article 520118

Siasa of Thursday, 24 December 2020

Chanzo: HabariLeo

Keisha aanza ziara kusikiliza changamoto za walemavu

Keisha aanza ziara kusikiliza changamoto za walemavu

MBUNGE wa viti maalum Khadija Shabani maarufu ‘Keisha’ ameanza ziara ya kutembelea walemavu na kubaini changamoto zao ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mwanzo wa vikao vya Bunge la 12 mwakani.

Keisha amesema lengo ni kupokea maoni yao, ushauri wao na nasaha zao, kuweka kwa pamoja mikakati na mipango endelevu, ili yeye akiwa kama mwakilishi wao Bungeni kwa kushirikiana na wao, Serikali pamoja na wadau wote waweze kufanikisha kuendelea kutatua changamoto za watu wenye ulemavu Tanzania.

“Mbali na kubaini changamoto zao pia nimekabidhi misaada kwa wenzangu wenye ulemavu pamoja na vitu vingine ikiwemo viti vyenye magurudumu (Wheelchairs).

Join our Newsletter