Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 09 25Article 510388

Siasa of Friday, 25 September 2020

Chanzo: Millard Ayo

Mambo 10 aliyozungumza Polepole "waungane watajua tulipotoka"

Mambo 10 aliyozungumza Polepole "waungane watajua tulipotoka"

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole leo September 24, 2020 amezungumza na waandishi wa habari, millardayo.com inakusogezea mambo 10 aliyozungumza.

“Mimi natoa rai wasisubiri Oktoba 3 ili waungane, hawa waungane sasa halafu ndiyo watajua tulipotoka na tulipofika na Watanzania, sisi tumeingia nchi hii ni maskini huyu mzee Magufuli kapambana leo sisi ni nchi ya uchumi wa kati” Polepole

“Yule mgombea wa chama cha bwana Zitto kule Zanzibar tutamshinda katika namna ambayo watu wake wa karibu wakae naye karibu, kwa sababu ushindi wa kipindi hiki utakuwa ni mkubwa mno kiasi kwamba wakae karibu  kumtia moyo” Polepole

“Kama Watanzania wangepiga kura Jumatano iliyopita, Septemba 23 mwaka huu, mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi, Dkt. Magufuli angeshinda kwa asilimia 89.5? Polepole

“Katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt. John Magufuli, pato la taifa ni shilingi trilioni 124 kwa mwaka. Hii ni hatua kubwa katika maendeleo” Polepole

“Majimbo ilikuwa ni sera ya kikoloni yenye lengo la kutugawa ili kutuongoza kikabila, yule mgombea wa chama cha Freeman Mbowe tangu ameenda kutibiwa kwa wakoloni amerudi na sera za kikoloni” Polepole

“Anasema kuwa viwanja vya ndege ujenzi wake na ukarabati ni anaamua mtu mmoja tu, hata kama yeye hakuwepo wenzake hawamwambii? Bunge lilipitisha bilioni 89 mwaka 2017/18 kwa kazi hiyo, mwaka 2018/19 bilioni 115, mwaka 2019/20 bilioni 40 na mwaka 2020/21 bilioni 60” Polepole

“Juzi bwana huyu anasema uwanja wa ndege wa Mpanda una nyasi na hautumiki. Uwanja wa Mpanda unafanya kazi hadi leo asubuhi na unatumiwa kwa kiasi kikubwa ni raia wa kigeni, dhamira yake ni nini huyu mgombea kwa watu Katavi kusema uwanja wa ndege hautumiki” Polepole

“Reli ya Kati ni reli kongwe, chini ya uongozi wa Rais, uzito wa reli hiyo ilikuwa ni ratili 50-60 tumeongeza uzito na kufikia ratili 70-80 ambapo inawezesha garimoshi kukimbia kwa mwendokasi wa 70-80 kwa saa” Polepole

TAJIRI NAMBA 1, TRILIONEA, ALIGAWA DHAHABU KAMA PIPI, WALINZI ELFU 60, MSAFARA TEMBO 100, NGAMIA 80

Join our Newsletter