Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 03Article 513790

Siasa of Tuesday, 3 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Mbowe, wenzake 13 washikiliwa kwa kupanga maandamano Dar

Mbowe, wenzake 13 washikiliwa kwa kupanga maandamano Dar

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 14 kwa kosa la kufanya mipango ya kuhamasisha maandamano bila kufuata sheria na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni; Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe pamoja na Tundu Antipas Lissu (aliyekuwa mgombea urais na makamu mwenyekiti chama hicho.

Mambosasa amewataja wengine kuwa ni; aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob , Godbless Lema (aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini), Denis Vesta, Godfrey Seleman, Elisha Mbandamka, Shehebu Kiarus, Yohana Marco, Salehe Omary, Mohamed Omary, Moses Omary, Charles Renatus na Essau Bwiru.

Kamanda huyo amesema, “Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na kati yao watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiliwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.”

Hata hivyo Kamanda huyu amesema kuwa jiji la Dar es Salaam kwa sasa lipo shwari na wanasiasa waache tabia ya kufanya fujo na kwamba wafuate sheria kwa kupeleka malalamiko yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kushawishi watu kufanya maandamano haramu yanayohatarisha maisha ya watu na mali zao.

Join our Newsletter