Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 12Article 518273

Siasa of Saturday, 12 December 2020

Chanzo: HabariLeo

Mbunge Musoma Vijijini kugawa majembe 50 ya kukokotwa na ng'ombe

Mbunge Musoma Vijijini kugawa majembe 50 ya kukokotwa na ng'ombe

VIKUNDI 50 vya wakulima vya jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, vinatarajia kupata mgawo wa majembe 50 ya kukokotwa na ng'ombe, yatakayotolewa na mbunge wa jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo.

Akizungumza na gazeti hili jana Profesa Muhongo alisema, atagawa majembe hayo wakati wa sikukuu ya Krismasi, ikiwa ni sehemu ya programu yake ya kutaka kupunguza matumizi ya jembe la mkono jimboni mwake.”

“Nilianza programu tangu Desemba mwaka jana ikiwa ni sehemu ya lengo kuu la kuboresha kilimo ndani ya vijijini 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini, kwani nilishagawa majembe 85 kwa vikundi mbalimbali," Profesa Muhongo.

Alifafanua kuwa anataka angalau kila kijiji kinakuwa na plau 20 ili iwe chachu ya kuhamasisha wakulima kuachana na jembe la mkono ambalo alidai linachelewesha maendeleo yao.

“Awali ratiba yangu ilikuwa ni kuyagawa majembe hayo 50 wakati wa sherehe za wakulima Nanenane mwaka huu, lakini kutokana na taratibu za uchaguzi ikabidi niahirishe hadi Desemba," alisema.

Aidha, alisema wakulima wameshaelezwa jinsi ya kupata mikopo ya kununua matrekta na kwamba ofisi ya Kilimo ya Halmashauri ya Musoma ipo tayari kuwasaidia kutuma maombi ya mikopo yao.

“Binafsi nimeshawagawia mbegu bora kwa wakulima jimboni mwangu zikiwamo za alizeti tani 20 mihogo, mtama na ufuta ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuboresha kilimo," alisema.

Mbunge huyo alisema wakulima wa jimboni mwake wanaongozwa na kaulimbiu za Kilimo ni 'Uhai, Kilimo ni Ajira na Kilimo ni Uchumi' ambazo zinwahamasisha kuboresha shughuli zao za kilimo.

Join our Newsletter