Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 21Article 515485

Siasa of Saturday, 21 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Mchujo mkali CCM mameya, wenyeviti

Mchujo mkali CCM mameya, wenyeviti

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imethibitisha majina ya wagombea wa nafasi za mameya wa majiji, Manispaa, Wenyeviti wa Halmashauri za wilaya na Halmashauri za Miji.

Uteuzi wa majina hayo umeelezwa haukuwa rahisi kwani katika maeneo mengine, licha ya kuwapo majina mengi, limerudi jina moja au mawili kulingana na matakwa ya Kamati Kuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema chama kimefanya mchujo kuhakikisha kinapata viongozi watakaokwenda na kasi ya utendaji kama ilivyo kwa Rais John Magufuli.

Polepole alisema Kamati Kuu ilikutana juzi, jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Alisema zipo baadhi ya Halmashauri za miji na wilaya ambazo watatakiwa kurudia uchaguzi mara moja kulingana na matakwa ya chama ili kufanya kazi hiyo vizuri zaidi na kwa tija.

Halmashauri hizo ni pamoja na Kilolo , Mufindi, Mpanda, Mtwara, , Nyasa, Msalala, Njombe, Geita na Nzega.

“Katika kipindi hiki CCM inataka kufanya mambo yake kivingine ambapo viongozi wa halmashauri zote ni lazima Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu iwathibitishe kabla ya kwenda kwenye mabaraza yao,” alisema Polepole nakuongeza kuwa kazi kubwa iliyopo ni kuchapa kazi kwa kasi.

Alisema lengo la Kamati Kuu Kuthibitisha majina hayo ni pamoja na kuangalia viongozi watakaokwenda na kasi ya Rais Magufuli ili wasiwe na mashaka nao, wawe ni wenye maadili, wachapa kazi, wasiwe wabadhirifu au wala rushwa bali wawe waaminifu, wanyenyekevu wakiweka mbele maslahi ya wananchi.

“Kipindi hiki hatutokuwa na mzaha kwa viongozi watakaoshindwa kutatua kero za wananchi, viongozi hawa ambao wanaenda kwenye mchakato wa mwisho mnayo kazi kubwa ya kufanya, wekeni maslahi ya watu mbele,” alisema na kuongeza kuwa kwenye Halmashauri kuwa ndipo fedha zinakwenda, hivyo waweke maslahi ya watu mbele.

Alisema viongozi watakaofanya vyema watavuka lakini wale wasioweza wakae pembeni.Yeyote atakayepatikana Kamati Kuu imejiridhisha.

Alisema baada ya uchaguzi kukamilika kuna kazi moja kwa Watanzania kipindi hiki ni kuchapa kazi na kuwapatia utumishi uliotukuka na kuandika historia ambayo CCM imepata kwa ushindi.

Alisema fedha nyingi ya maendeleo huenda katika halmashauri kwa ajili ya maendeleo, ambapo wananchi hushiriki moja kwa moja kwa ajili ya kupanga mambo mbalimbali ya maendeleo.

Polepole aliwataka viongozi watakaochaguliwa kutambua kwamba wanayo kazi kubwa ya kufanya huku wakiweka mbele maslahi ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao.

Akianisha nafasi za uteuzi wa umeya kwa jiji la Dar es Salaam wagombea walikuwa tisa, Arusha 17, Dodoma saba, Tanga sita, Mwanza saba na Mbeya wagombea 10.

Wagombea wa nafasi ya Meya wa Manispaa walijitokeza 150 kati ya nafasi 20 na wenyeviti wa Halmashauri za wilaya 137 walijitokeza wagombea 682. Na nafasi za Wenyeviti wa Halmashauri za Miji ni nafasi 22 huku wagombea wakiwa 109.

Waliothibitishwa kugombea nafasi ya Umeya kwa jiji la Dar es Salaam ni Mariam Mohamed, Adinan Kondo na Omar Matulanga . Kwa Jiji la Arushala , wagombea ni Maxmillian Irank, Prosper Msoffe na Isaya Doita.

Katika majiji mengine, kwa upande wa Dodoma kamati kuu imerejesha jina moja la Profesa Davis Mwamfupe. Mbeya waliorejeshwa ni Daud Nelson , Noor Mohamed na Daniel Yesaya, Mwaza Biku Kotecha Edith Emil na Sima Costantine.

Kuhusu Meya wa Manispaa, kwa Manispaa ya Ubungo ni Esta Ladislaus na Jafary Nyaigesha; Kigamboni ni Ernest Mafimbo; Kinondoni ni Leonard Manyama na Songoro Mnyonge; Ilala ni Omary Said Kumbila moto; Temeke ni Juma Rajab na Abdallah Mtinika.

Pamoja na majina hayo, alisema Kamati Kuu imetoa pongezi kwa Uteuzi wa Makamu wa pili wa Rais kwa serikali ya Zanzibar .

Join our Newsletter