Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 24Article 515957

Siasa of Tuesday, 24 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Mdee aahidi jambo kwa Spika wabunge Chadema wakiapishwa

Mdee aahidi jambo kwa Spika wabunge Chadema wakiapishwa

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amemhakikishia Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa atampa ushirikiano wakati akitekeleza majukumu yake katika Bunge la 12.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake 18 walioapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chadema jijini Dodoma leo, Jumanne, Mdee amesema nafasi hizo kuwa si hisani kwa chama chake bali zinatokana na ushindi mkubwa kwa chama hicho.

" Spika tumefanya kazi wote kwa miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa uadilifu mkubwa…tuna vijana wapya na sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi nzuri kwa ajili ya Taifa hili," amesema Mdee.

Katika hafla ya kuapisha wabunge wateule wa viti maalum, wengine walioapishwa ni aliyekuwa mbunge Ester Bulaya, Esther Matiko, Grace Tendeka, Ester Bulaya, Kunti Yusuf, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo,Nusrat Hanje, Agnesta Lambat, Sophia Mwakagenda, Cecilia Pareso, Jesca Kishoa, Ester Bulaya, Naghenjwa Kaboyoka.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ifakapo Februari 02, 2021 atatolea ufafanuzi juu ya zoezi hilo la kuapisha wabunge hao na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wabunge hao katika kutekeleza majukumu yao.

Join our Newsletter