Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 09 25Article 510397

Siasa of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Mgombea CCM aomba kuchaguliwa tena

Mgombea CCM aomba kuchaguliwa tena

MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amewaomba wakazi wa kata ya Mirongo waweze kumchagua tena ili aweze kuwaletea maendeleo.

Mabula alisema hayo wakati alipokuwa katika mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Ngokozi katika kata ya Mirongo.

Alisema katika mwaka 2015 jiji la Mwanza lilikuwa likipokea Sh bilioni 2 katika sekta ya Elimu bila malipo na kwa sasa Mwanza inapokea Sh bilioni 9.

Alisema katika miaka mitano (2015-2020) Serikali imefanikiwa kutengeneza madawati 31,000 kwajili ya shule ya msingi na sekondari na wametenga Sh milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza madawati 250 katika shule ya sekondari ya Mirongo.

Mabula alisema katika mradi wa Maji taka jumla ya Sh bilioni 1.2 imetumika katika mradhi huo na wakazi 1,500 wamenufaika haswa kutoka maeneo ya kata za Igogo, Isamilo, Pamba, Mabatini na Mbugani.

Join our Newsletter