Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 10 30Article 513448

Siasa of Friday, 30 October 2020

Chanzo: HabariLeo

Mwana FA ashinda Muheza Yosepher agoma kusaini

Mwana FA ashinda Muheza Yosepher agoma kusaini

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimendeleza wimbi la ushindi wilayani Muheza ambapo mgombea ubunge Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ ametangazwa kuwa mshindi kwa kura 47,578 na kumuacha mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 12,036 kati ya kura halali 61,391 zilizopigwa.

Mbali na vyama vya CCM na Chadema,vyama vingine vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi huo katika nafasi ya ubunge ni (CUF) ambapo mgombea wake Juma Nindi amepata kura 362 ,Jamila Ally wa ACT-Wazalendo amepata kura 1,223 na Mhina Mhina wa (UDP) amepata kura 194.

Akitangaza matokeo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, Nasib Mbaga amesema watu waliojiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga kura jimboni humo ni 140,489 ambapo waliopiga kura ni 63,268,kura halali ni 61,391 na kura zilizoharibika ni 1,877 na vituo vya kupigia kura jimboni humo vilikuwa 437.

Amesema kuwa katika nafasi za udiwani jimbo hilo lenye jumla ya kata 37, kati ya hizo 35 zimekwenda kwa CCM na kata mbili za Mkuzi na Potwe zimechukuliwa na CHADEMA.

Kuhusu kuchelewa kutangaza matokeo ambayo amatangaza majira ya saa 1:50 usiku wa jana ametaja sababu kuu mbili ambazo ni hali ya hewa ya mvua iliyonyesha ka siku mbili mfululizo ambapo kutokana na jiografia ya Wilaya ya Muheza kuna baadhi ya maeneo katika Tarafa ya Amani,kata za Kambai, Kwezitu Potwe ,Tongwe,Nkumba,na Kigombe njia ziliharibika zikawa hazipitiki hivyo matokeo ya kata hizo yalichelewa kufika katika kituo cha majumuisho ya kura jimboni ambapo matokeo ya mwisho yalifika majira ya saa 6:57 mchana.

Amesema sababu nyingine ni mgombea ubunge kupitia tiketi ya Chadema,Yosepher Komba kutaka matokeo hayo yarudiwe kuheasbiwa jambo ambalo limeplekea kuchelewa kutangaza.

Kwa upande wake mbunge mteule wa jimbo hilo,Hamisi Mwinjuma aliwashukuru wananchi wa Muheza kwa kumpa ushindi na kusema kuwa wamemkopesha kura ila yeye atawalipa maendeleo.Kwa upande wake,Yosepher Komba amesema kuwa amechezewa ‘rafu’ hivyo amegoma kusaini.

Join our Newsletter