Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2021 01 05Article 520490

Siasa of Tuesday, 5 January 2021

Chanzo: HabariLeo

Mwigulu ataka utafiti kujua wapigakura Iramba Magharibi

Mwigulu ataka utafiti kujua wapigakura Iramba Magharibi

MBUNGE wa Iramba Magharibi, Dk Mwigulu Nchemba (pichani) amesema upo umuhimu wa kufanya utafi ti kujua ni kwanini pamoja na ushindi mkubwa iliopata CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, watu waliopiga kura walikuwa wachache jimboni humo.

Amesema idadi ya wapigakura asilimia 30.34 isiyofika nusu ya watu 141,521 waliojiandikisha jimboni humo ilikuwa ni ndogo ikilinganishwa na wapigakura waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Dk Mwigulu alisema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM wilayani humo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Kiomboi hivi karibuni. “Hili ni jambo la kufanyiwa kazi kwa haraka kwani katika tathmini za kiushindani linapaswa kupatiwa majibu ikiwamo kubaini chanzo cha tatizo hilo.”

“Tumeshinda kwa kiwango kikubwa kwenye nafasi ya urais, mbunge na madiwani lakini kuna kiporo cha kukifanyia kazi kwani idadi ya watu waliojitokeza kupigakura ni ndogo kuliko ya waliojiandikisha,” alisema.

Katika kikao hicho, Dk Mwigulu ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria alitunukiwa vyeti viwili vya pongezi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuimarisha chama na ushiriki wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Dk Mwigulu amewasihi Watanzania kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli kwani rekodi ya utendaji kazi aliyofanya kwa wananchi wa Tanzania katika huduma mbalimbali za kijamii haina kifani na itatumika kama somo duniani kote.

“Ingekuwa imepitishwa kuwa na Rais mmoja wa Afrika ni wazi kuwa Tanzania tungekuwa tumetoa Rais huyo ambaye ni Dk John Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya,” alisema Mwigulu.

Join our Newsletter