Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 12Article 518207

Siasa of Saturday, 12 December 2020

Chanzo: Zanzibar 24

NDUGAI AWANYOSHEA KIDOLE WABUNGE WA ACT

NDUGAI AWANYOSHEA KIDOLE WABUNGE WA ACT

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemuapisha Prof. Shukrani Manya kuwa mbunge rasmi na kutoa wito kwa wabunge wa ACT Wazalendo kutoa taarifa ili wapangiwe kuja kuapishwa na kuwatumika wananchi wao.

” Tuna wabunge wa ACT-Wazalendo wanne ambao bado hawajaapa, ningependa kutoa wito na wenyewe wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi, hawana sababu ya kuendelea kuzurula huko waliko, watoe taarifa kwa spika haraka tuwapangie ili wapate kiapo”

Nitoe wito kwa wabunge wengine wowote wale, kumbukumbu zangu zinaonesha kuna wabunge wanne wa ACT Wazalendo ambao bado hawajaapa ningetoa wito kama wenyewe wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi hawana sababu ya kuzurura huko walipo watoe taarifa kwa spika haraka tuwapangie ili wapate kiapo waweze kufanya kazi ya mbunge” amesema Ndugai

Spika ndugai amesema hayo  mara baada ya kiapo cha Prof. Manya jijini Dodoma leo.

Join our Newsletter