Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 30Article 516764

Siasa of Monday, 30 November 2020

Chanzo: Zanzibar 24

NDUGAI:HALIMA MDEE NA WENZIWE NI WABUNGE KAMILI

NDUGAI:HALIMA MDEE NA WENZIWE NI WABUNGE KAMILI

“Waliokuwa na wasiwasi kuhusu wale Wabunge 19 (Halima Mdee na wenzake) sijui kuna hili kuna hili, niwatoe wasiwasi wale ni Wabunge kamili, na Wanahabari mkiwaandika muwaite Waheshimiwa”-Spika wa Bunge, Job Ndugai

“Watanzania tupige vita na tukatae ukandamazaji dhidi ya Wanawake kwenye Jamii yetu kwa kisingizio chochote, Mbowe ni Rafiki yangu amesimama akaanza kuwatukana hadharani Wabunge hawa Wanawake ni aibu kuwatukana Wanawake hadharani”-NDUGAI

“Mbowe umesahau Mdeee alivunjika mkono kwa ajili ya kukufuata Magereza, Bulaya apigwa akazimia amepelekwa Aga Khan kwa ajili yako Mbowe, Matiko amelazwa Segerea mara nyingi kwa ajili yako, mshahara wao kuwafukuza hadharani bila kuwasikiliza, haiwezekani”-NDUGAI

Join our Newsletter