Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 03Article 513778

Siasa of Tuesday, 3 November 2020

Chanzo: Millard Ayo

Ndugai achukua fomu kutetea kiti cha Spika (+picha)

Ndugai achukua fomu kutetea kiti cha Spika (+picha)

Leo November 3, 2020 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Job Ndugai amechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la 11 amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika Ofisi Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma. Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.

Aidha Itunda amesema kuwa fomu hizo zinatolewa kwa gharama ya Sh 500, 000 na zoezi hili litafikia kikomo leo saa 10 jioni.

UWEZO WA KOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI

Join our Newsletter