Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 16Article 518798

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 16 December 2020

Chanzo: habarileo.co.tz

Ndugai bega kwa bega na wabunge ACT Wazalendo

Baada ya leo kuwaapisha wabunge wateule wa chama cha ACT Wazalendo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amewahakikishia kuwa atawahapa ushirikiano na kusikiliza maoni na ushauri wao.

Akizungumza katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema atahakikisha analinda haki za wabunge hao ikiwemo kuwasikiliza, kupokea maoni na ushauri wao.

“Ni wajibu wa Spika kuhakikisha walio wachache wanapata haki ya kusikilizwa na kama hoja itakuwa nzito basi walio wengi wataamua lakini haki ya kusikilizwa itakuwepo,” amesema Ndugai.

Aidha, amesema Kwa kutambua kuwa watanzania wanapenda kusikia bajeti zikipangwa kwa kutoa, basi watafanya hivyo kwa weledi na kufanya maamuzi bora kwa maslahi ya taifa.

“Uchaguzi umeisha, uchaguzi ule wa Oktoba 28 umekwisha, sasa tusonge mbele, tufanye kazi tukimsaidia Rais kwa maslahi ya taifa hili”ameongeza Ndugai

Amesema hadi sasa kuna idadi ya wabunge 383 ambao wameampishwa, bado wabunge 10 ili kolamu ya bunge itimie na kufanya maamuzi.

Wabunge hao 10 ni wale watano ambao ni wa kuteuliwa na Rais, na watano ni wale wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Join our Newsletter