Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 19Article 519512

xxxxxxxxxxx of Saturday, 19 December 2020

Chanzo: millardayo.com

Nyumba yateketea kwa moto Mbeya, Dr. Tulia afika kutoa pole (+picha)

December 19, 2020 Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amefika kuwapa pole na kujionea athari zilizotokea baada ya nyumba ya familia moja kuteketea kwa moto asubuhi ya leo katika kata ya Majengo Jijini humo ambayo hadi sasa bado haijabainika chanzo kamili cha ajali hiyo.

Akiongea na wahanga pamoja na majirani wa familia hiyo Dr. Tulia amesema>>>’’Niwape pole kwa hii changamoto mliyokumbana nayo, kwa sasa hatuwezi kuzungumza mengi kwa sababu kila mtu sasa yupo katika hali ya masikitiko na hata tathimini inaweza kuwa ngumu kwa sasa kufanyika lakini ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha”

“Hizi mali zinatafutwa lakini uhai hautafutwi hivyo licha ya kupoteza kila kitu kwa kuteketezwa kwa moto hatuna budi kushukuru kwa uhai, kwahiyo niwaombe pamoja na hii changamoto basi mtulize moyo. Sasa katika hali hii wakati tukisubiri kuona nini cha kufanya nikitoka hapa nitawaagiza vijana wangu wawaletee chakula na pesa kidogo kwa ajili ya kujikimu kidogo kwa hizi siku kadhaa”- Dr. Tulia Ackson

“Sote tunafahamu ajali haipigi hodi hivyo katika hilo nitumie fursa hii kuwaomba pia majirani zetu wengine mwenye chochote kwa ajili ya hawa ndugu zetu basi anaweza kukiwasilisha ili tuwasaidie, kama tulivyojionea kila kitu hapa kimeteketea hivyo tuendelee kuwafariji huku tukiwaombea hawa ndugu zetu utulivu wa moyo”-Dr. Tulia Ackson

DUUH!! WAZIRI MKUU AWASHA MOTO “MNANIDANGANYA, HOVYO KABISA HAPA HAKUNA WATUMISHI HAMISHA”

Join our Newsletter