Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 02Article 513613

xxxxxxxxxxx of Monday, 2 November 2020

Chanzo: millardayo.com

Prof. Lipumba "hatutakula na tutafanya dua"

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametangaza kuwa kutokana na uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa nchini, chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote.

Lipumba ameyasema hayo Makao Makuu ya Ofisi za CUF,  Jijini DSM, ambapo ameeleza kuwa sasa watajikita katika harakati za kudai Katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi.“CUF tunawaomba watanzania wote wapenda haki kuungana na sisi katika ibada siku ya Alhamis, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kuomba hukumu ya haki kutokana na kile kilichofanyika” Prof. Lipumba.

 “Hatukubaliani na matokeo kwasababu tumeibiwa sana, mfano Jimbo la Temeke mgombea wetu wa Ubunge katika kituo alichopiga kura yeye na familia yake amepata kura sifuri ina maana hata mwenyewe hakujichagua” Prof. Lipumba

UWEZO WA MAKOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI

Join our Newsletter