Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 10 29Article 513379

Siasa of Thursday, 29 October 2020

Chanzo: Millard Ayo

Profesa Mkenda ashinda Ubunge Jimbo la Rombo

Profesa Mkenda ashinda Ubunge Jimbo la Rombo

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Rombo Godwin Chacha amemtangaza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha Ubunge kwa kupata Kura 48,120 dhidhi ya mpinzani wake Patrick Asenga wa CHADEMA aliyepata kura 9519.

Wagombea wengine ni Jafett Massawe wa ACT aliyepata kura 1564, Jubicate Tahayo CUF kura 107, Michael Clemence TLP kura 167 na Joseph Selasini NCCR Mageuzi kura 416 ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake kwa Jimbo hilo.

Jumla ya wapiga kura Waliojiandikisha walikuwa 146070 ambapo Kura zilizopigwa ni 610,11 ambapo 1216 ziliharibika.

LIVE: MOSHI MJINI MSHINDI NI PRISCUS TARIMO

Join our Newsletter