Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 03Article 517127

Siasa of Thursday, 3 December 2020

Chanzo: HabariLeo

Ridhiwan kumaliza shida ya maji Chalinze

Ridhiwan kumaliza shida ya maji Chalinze

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa shida ya maji katika Kata ya Kibindu jimboni humo itakuwa historia kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji itakayogharimu shilingi bilioni 1.6.

Ridhiwani amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwamduma kilichopo katika kata hiyo wilayani Chalinze, mkoani Pwani.

Aidha, Mbunge huyo amewahakikishia wananchi hao kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati ili kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama.

“Mimi kama Mbunge nimeshafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuchimba visima vinne katika vijiji mbalimbali kwenye kata hii ambavyo kwa kiasi chake vimesaidia ingawa shida ya maji bado ipo” amesema Ridhiwani.

Join our Newsletter