Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 01Article 516779

Siasa of Tuesday, 1 December 2020

Chanzo: HabariLeo

SPIKA Ndugai aonya viongozi wa siasa wanaodhalilisha Bunge

SPIKA Ndugai aonya viongozi wa siasa wanaodhalilisha Bunge

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameonya viongozi mbal- imbali wa vyama vya siasa wanaodhalilisha Bunge hadharani, akisema vitendo hivyo havikubaliki katika jamii.

Akizungumza katika Viwanja vya Bunge jana baada ya kuwaapisha Wabunge wa Kuteuliwa na Rais John Magufuli, Humphrey Polepole na Riziki Lulida, Spika Ndugai alikemea vitendo hivyo vya kudhalilisha Bunge hadharani pamoja na wabunge kwamba havi- kubaliki na hatua zitachukuliwa kwa wanaofanya hivyo.

Aliwaonya watu wanaodhalilisha, kubeza na kudharau wabunge, Bunge na wabunge walioapa.

Alisema hatakubali kuona vitendo hivyo vikiendelea.

Aidha, Spika Ndugai alisema kuwa wabunge 19 wa Viti Maalu- mu wa Chama cha Demokrasia na

Maendeleo (Chadema) aliowaapi- sha hivi karibuni, ni wabunge halali kama ilivyo kwa mbunge mwingine wa chama hicho wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenan.

Kuhusu malalamiko kwa nini anaapisha wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge, Spika Ndugai alisema hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 30 (2) b ya Bunge ambazo zime- anza kutumika katika Bunge la 12 zinazomruhuru kuapisha wabunge sehemu yoyote nje ya Ukumbi wa Bunge wakati hakuna mikutano inayoendelea.

Spika Ndugai alisema Novemba 29, mwaka huu alipokea barua kutoka kwa Rais Magufuli kuhusu kuteuliwa kwa Lulida na Polepole kuwa wabunge wa kwanza katika nafasi zake 10.

Alisema katika orodha hiyo, bado rais anazo nafasi nyingine nane zilizobaki na akikamilisha na kupata pia wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, idadi ya wabunge 393 itatimia.

Akizungumza baada ya kuapa, Polepole aliyekuwa Katibu wa Hal- mashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Itikadi na Uenezi, alimshukuru Rais Ma- gufuli kwa kumpa nafasi hiyo na kuwa sehemu ya Bunge na akas- ema atachukua muda kujifunza.

Lakini aliahidi kuwa atatumia nafasi yake kama mbunge kusaidia umma na chama chake kuhakiki- sha ahadi walizotoa kwenye kampeni kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya CCM anasimamia ipasavyo ili zinatekelezwe.

Naye Lulida alisema anamshu- kuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa mbunge, akiahidi atafanya kazi kwa kwa moyo wake wote, uaminifu na kuhakikisha anaiten- dea haki nafasi yake hiyo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kwa tiketi ya CCM, Jacquiline Ngonyani aliwaahidi wabunge wa Viti Maalumu Chade- ma kuwa watashirikiana nao na watahakikisha haki zao wanapata.

Wakati huohuo, Baraza la Wazee la Chadema (BAZECHA) Mkoa wa Dar es Salaam limeunga mkono hatua ya Kamati Kuu ya chama hicho kuwavua uanachama wabunge wa Viti Maalumu 19 walioapishwa hivi karibuni.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa baraza hilo, Uhuru Moshi alidai kitendo kilichofanywa na waliokuwa wana- chama wenzao na baadhi viongozi ni usaliti kwa chama hicho.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamati Kuu ya Chadema iliwavua unachama pamoja na nyadhifa zao wabunge wa Viti Maalumu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWA- CHA), Halima Mdee, kwa madai kuwa walifanya usaliti baada ya kwenda kuapa, bila kuzingatia misingi ya chama hicho. Mbali na hilo, Moshi ali-

washauri wajumbe wa Kamati Kuu kutoishia hapo badala yake kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu wote waliohusika na mchakato huo wa kupatikana kwa wabunge hao 19 hadi kwenda kuapishwa.

Wabunge hao wanadaiwa kuvuliwa uanachama ni Mdee, Esther Matiko, Ester Bulaya, Nag- enywa Kaboyoka, Grace Tendega, Cecilia Paresso, Jesca Kishoa na Hawa Mwaifunga.

Wengine ni Tunza Malapo, Sofia Mwakagenda, Kunti Ma- jala, Antropia Teonjest, Salome Makamba, Conchesta Mwamlaza, Agnesta Kaizer, Nusrat Hanje, Felister Njau, Asia Mwadini Mo- hamed na Stella Fiao.

Imeandikwa na Magnus Mahenge, Dodoma na Oscar Job, Dar.

Join our Newsletter