Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2021 01 15Article 521237

Siasa of Friday, 15 January 2021

Chanzo: HabariLeo

Seif Sharif Hammad: Hakuna lisilo wezekana

Seif Sharif Hammad: Hakuna lisilo wezekana

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharifu Hamad, amesema wale waliodhani kisiwa hicho hakiwezi kuwa na serikali ya Umoja wa Kitaifa watambue limewezekana na kuwa wamekubaliana na wana dhamira ya kweli yeye na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuwaunganisha wazanzibari.

Kauli hiyo aliitoa leo muda mfupi uliopita, Chato mkoani Geita walipotembelea Soko la Kimataifa la samaki na dagaa la Kasenda lililo katika Kata ya Mganza wilayani humo.

Maalim Seif amesema hakuna lisilowezekana ikiwa pande zote zina nia na dhamira ya dhati ya kuwaunganisha Wazanzibari na kwamba yeye pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi wameweka tofauti za kisaasa kando na kuwaunganisha wananchi .

“Ziara ya Chato imekuwa na mafanikio kwa sababu yale tuliyoyajia ya kuzungumza na Rais John Magufuli yamefanikiwa kwa kiwango cha juu na hilo ni furaha kwetu,” amesisitiza

Kwa upande wa Rais Mwinyi akizungumzia kuinua uchumi wa Zanzibar kupitia uchumi wa bluu unaotegemea bahari, Rais wa visiwa hivyo, amesema ziara yao hiyo imekuwa na manufaa mengi kwani Zanzibar inategemea zaidi bahari kwa ajili ya kuinua uchumi

Join our Newsletter