Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 12 08Article 517694

Siasa of Tuesday, 8 December 2020

Chanzo: HabariLeo

Uchaguzi serikali za mitaa Feb. 6

Uchaguzi serikali za mitaa Feb. 6

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepanga uchaguzi wa serikali za mitaa kuanza Februari 6 na kukamilika Machi 2 mwakani baada ya ratiba hiyo kupitishwa na Baraza la Mawaziri.

Akizngumza na gazeti la The New Times juzi, Katibu Mtendaji wa NEC, Charles Munyaneza alisema viongozi wa sasa wa serikali za mitaa wanamaliza muda wao mwakani baada ya kutumikia wananchi kwa miaka mitano kuanzia 2016 na kukamilika Februari 2021.

Alisema uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia taratibu za kujikinga na corona ikiwamo kuzingatia umbali baina ya mtu mmoja na mwingine.

“Tumepanga kuwa na takribani vituo vya kupiga kura viwili kwa kila kijiji, lakini idadi ya wakazi wa maeneo hayo watafanya maamuzi ili kuhakikisha suala la umbali linaheshimika katika vituo vyote vya kupiga kura,” alisema

Alisema pia kutakuwa na vituo vya kunawa mikono katika kila eneo pamoja na vitakasa mikono kwa wapigakura kabla na baada ya kupiga kura.

Munyaneza alisema NEC itatumia faranga bilioni 3.3 kwa ajili ya uchaguzi huo wa mabaraza ya ushauri katika vijiji na wilaya, makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Wagombea wanatarajiwa kuwasilisha fomu za kugombea kuanzia Desemba 28 hadi Januari 11 na NEC itafanya uhakiki kwa wapigakura kuanzia Januari 11 hadi 22.

Join our Newsletter