Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 19Article 515191

Siasa of Thursday, 19 November 2020

Chanzo: Millard Ayo

Wanawake watatu waachwa na waume zao kisa siasa "wapo CCM waume ACT" (+video)

Wanawake watatu waachwa na waume zao kisa siasa "wapo CCM waume ACT" (+video)

Wanawake watatu wamethibitika kupewa talaka na Waue zao baada ya hekaheka za uchaguzi, huko katika Jimbo la Wete mume amemuacha Mkewe Bi. Zawadi Ally Haji.

“Niliachwa kipindi hicho cha siasa, Mume aliniambia nikienda kupiga kura ndio talaka yangu na mimi nikaenda, nilivyorudi jioni ndio nikawa nishaachika, nilipokwenda nikamchagua Rais ninaemtaka mie” Bi Zawadi

“Hussein na Salim Mussa, kwa sababu ndio yeye hakuwataka sikumfuata upande wake atakao, kwa sababu nimefata upande wangu ninaoutaka”  Bi. Zawadi, mke alieachika

Mzazi wa Bi. Zawadi, Zadi Hamad Iddy amesema kwa masikitiko binti yake huyo amerejea nyumbani akiwa na mtoto wake mdogo.

“Sijapokea uzuri kwa sababu alipoanza kumposa huyu ni mwali na mama yake alikuwa ni mwana CCM na alipokuja tulimwambia unakuja tuolea mwenetu lakini yuko upande wa CCM na huyu mwanaume alikuwa ni CCM” Zadi Hamad

“Baada ya kukaa na kugombana na wazazi wake akatoka CCM akajifanya CUF kwanza, baadae ndio akaja ATC lakini wakati wote huo hawana ugomvi lakini ikifika wakati wa siasa tu” Zadi Hamad

Join our Newsletter