Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 03Article 513787

Siasa of Tuesday, 3 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Zitto, Mdee watakiwa kujisalimisha Polisi

Zitto, Mdee watakiwa kujisalimisha Polisi

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wanasiasa Zitto kabwe na Halima Mdee kujisalimisha polisi kwaajili ya kuendelea na mahojiano kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa alisema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 14 waliokuwa wamepanga kufanya maandamano kinyume na taratibu za sheria na kwamba wanasiasa hao wawili (Zitto na Mdee) wanapaswa kutoa maelezo juu ya suala hilo.

“Tunawatafuta Halima Mdee ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia Chama cha Chadema pamoja na Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT wazalendo) aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini ili waweze ili kuendelea na mahojiano kwa tuhuma zinazowakabili,” alisema Mambosasa.

Watuhumiwa 14 wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni; Freeman Mbowe pamoja na Tundu Antipas Lissu (ameachiwa kwa dhamana). Boniface Jacob (aliyekuwa Meya wa Ubungo), Godbless Lema (aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini), Denis Vesta, Godfrey Seleman, Elisha Mbandamka, Shehebu Kiarus, Yohana Marco, Salehe Omary, Mohamed Omary, Moses Omary, Charles Renatus na Essau Bwiru.

Join our Newsletter