Uko hapa: NyumbaniInfosSiasa2020 11 03Article 513799

Siasa of Tuesday, 3 November 2020

Chanzo: HabariLeo

Zitto akamatwa, Mdee bado

Zitto akamatwa, Mdee bado

SAA chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutangaza kumsaka Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Jeshi hilo limemnasa mwanasiasa huyo wakati alipofika kwenye Kituo cha Polisi Osterbay, Dar es Salaam.

Zitto amekamatwa mchana wa leoo akiwa kituoni hapo alipokwenda kuwajulia hali, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, Boniface Jacob na wenzao wengine 10.

Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, Janeth Rithe amesema, “Ni kweli Zitto amekamatwa na polisi akiwa kituo cha polisi cha Oysterbay alikokwenda kuwaona viongozi wa Chadema.”

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa mapema leo alisema kuwa aliwataka wawili hao kujisalimisha polisi kwa mahojiano dhidi ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya kupanga maandamano.

Kukamatwa kwa Zitto kumembakisha Mdee, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

JALADA LA LISU LATUA KWA AG

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limepeleka jalada la kesi inayomkabili Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika 28 Oktoba 2020 kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara na wenzake wawili walikamatwa jana jioni Jumatatu Novemba 2, 2020 Ofisi za Umoja wa Ulaya (EU) jijini Dar es Salaam kisha kuhojiwa na kuachiwa.

“Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi,” Lazaro Mambosasa

Join our Newsletter