Uko hapa: NyumbaniHabariTaarifa Kwa Vyombo vya Habari2021 08 17Article 551998

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia Afanya Teuzi Mpya

Rais Samia Hassan Rais Samia Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othamn aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha cha Ardhi (ARU).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Agosti 17, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu imesema pia Rais Samia pia amemteua Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Profesa Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Profesa Ole Gabriel anachukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu. Profesa Ole Gabriel ataapishwa Agosti 21 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na mabalozi wateule watatu ambao ni:

Balozi mteule Luteni Jenerali Yakub Hassan Mohamed aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

Balozi mteule Mahmoud Thabit Kombo aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Balozi Mteule Elsie Sia Kanza aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.