Uko hapa: NyumbaniHabariTaarifa Kwa Vyombo vya Habari2021 08 17Article 551911

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa SADC

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan ni miogoni mwa Marais wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchiza kusini mwa Afrika,Unaofanyika nchini Malawi.

Mkutano huo wa 41 umeanza leo nchini humo katika mji wa Lilongwe, ambapo unatarajia kumalizika kesho.

Umehudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali wa jumuiya hiyo, akiwemo Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakiongozwa na mwenyeji wao Rais wa Malawi Lazarus Chikwera.

Malawi inapokea kijiti cha nafasi hiyo kutoka kwa nchi ya Msumbiji ambayo nayo ilipokea kijiti hicho kutoka Tanzania, kama ulivyo utaratibu wa jumuiya hiyo kupewa nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaaka mmoja.