Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 11 25Article 574060

Habari za Mikoani of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: ippmedia.com

Kilio cha wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kimemfikia RC Makalla

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Amos Makala Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Amos Makala

MKUU wa Mkoa wa MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, amesema pamoja na kup Amos Makalla, amesema pamoja na kupokea kwa kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia lakini pia kuna baadhi ya wanaume wenye changamoto hiyohiyo ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia na wanahitaji msaada pia.

Akizungumza leo Novemba 25, 2021 wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Makala amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko dhidi ya wanawake wenye fedha.

“Nilikuwa na ziara ya kusikiliza kero za wananchi, asilimia 30 ya kero 927 nilizopokea zinatokana na changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia."

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa, kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makalla.