Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 09 14Article 557365

Habari za Mikoani of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: Wasafifm

Madereva wa mabasi Njombe waweka mgomo

Madereva wa mabasi Njombe waweka mgomo Madereva wa mabasi Njombe waweka mgomo

Madereva wa magari yaendayo mikoa mbalimbali mkoani Njombe wamefanya mgomo wa kusafirisha abiria kwa takribani masaa matatu wakishinikiza kuachiwa kwa dereva mwenzao wa basi la Luwinzo ambaye alikamatwa na askari siku ya jana eneo la Makambako wakati akitokea Dar es salam na kuwekwa mahabusu kwa kosa la kutembea kwa mwendo kasi.

Madereva hao wamedai kuwa wamekuwa wakionewa mara kwa mara na askari wa barabarani ambapo askari hao wamekuwa wakiwapiga tochi kwa nyuma pamoja na kuwalipisha faini kubwa isivyo kawaida.

ASP Jane Warioba, Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Njombe aliwasili katika eneo la stendi kuu ya mkoa huo na kukutana na madereva hao ambapo amewaomba kuendelea na safari zao kama kawaida huku akiahidi kushughulikia tatizo lao.

Amesema miundombinu ya barabara za mkoa huo ni nyembamba na zenye miinuko ambazo zinawataka madereva kuendesha magari yao kwa tahadhari lakini wamekuwa wakiendesha kwa fujo bila kujali tahadhari hizo.