Uko hapa: NyumbaniInfosDini2020 09 25Article 510400

Regional News of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Mikoa 23 Tanzania Bara rasmi kuanza mabucha nyamapori

Mikoa 23 Tanzania Bara rasmi kuanza mabucha nyamapori

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imetangaza kuanza kwa bucha za kuuza nyamapori katika mikoa 23 ya Tanzania bara.

Kutangazwa rasmi kuwepo kwa bucha hizo ni baada ya kupata maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Rais John Magufuli mnamo Januari 3 mwaka huu (2020) wakati akiwa ziara ya kikazi Mkoani Rukwa.

Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Dk Aloyce Nzuki alitangaza hatua ya kuanzishwa kwa bucha hizo jana ( Sept 25) akiwa katika Ofisi za makao makuu ya TAWA yaliyopo mkoani Morogoro.

Dk Nzuki , alisema kuanzishwa bucha za kuuza nyamapori ni fursa kwa wananchi na ni matakwa ya Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007 na sheria ya kuhifadhi wanyamapori sura namba 283.

"Sheria hii imehimiza wananchi kutumia na kunufaika moja kwa moja au shughuli za utalii zinazoiletea Serikali mapato kupitia matumizi kwa endelevu ya rasilimali ya wanyamapori,"alisema Dk Nzuki.

Join our Newsletter