Uko hapa: NyumbaniInfosDini2019 11 16Article 488095

Regional News of Saturday, 16 November 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

Mke wa Rais Magufuli atoa misaada kwa wazee wa Nunge Dar

Mke wa Rais Magufuli atoa misaada kwa wazee wa Nunge Dar

Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao  New Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam Mama Magufuli ambaye aliambatana na mlezi wa umoja huo, Mary ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wake, Tunu ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa misaada mbalimbali ya ujenzi, chakula na nguo. Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa Sh5 milioni kwa ajili ya ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Ijumaa Novemba 15, 2019 kilikuwa na wazee 26. Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa kisima cha maji kwa gharama ya Sh1.9 milioni, vyakula na nguo vyenye thamani ya Sh3 milioni.

Join our Newsletter